WATENDAJI WAKUU IDARA YA MAJI WATAKUWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKUANO



📌NA HAMIDA RAMADHANI


KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amewataka watendaji wakuu katika idara za Maji kufanya kazi kwa ushirikiano kwa ajili kusaidia wananchi kupata huduma hiyo kwa uhakika.

Akifungua leo kikao kazi cha kutathimini utendaji kazi katika sekta ya Maji Mhandisi Sanga amesema kuja baadi ya watendaji wanafanya kazi bila ushirikiano hali ambayo inaounguza tija katika kutoa huduma hiyo kwa wananchi.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wakugenzi wote katika Idara za Maji waimarishe utendaji kazi unaozingatia ushirikiano na kufikia lengo la kuwahufumia wananchi.

Maeneo mengi bado kuna umimi,naomba umimi huu tuumalize,tushirikiane katika utendaji wetu kwa ajili ya kufanya kazi yetu owe bora zaidi katika kuwatumikia wananchi.
Mhandisi Sanga

Aidha amewataka watendaji hao kila mmoja kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana katika eneo lake .

Kila mmoja naomba ajiulize maswali matatu je katika eneo langu wananchi wanapata huduma bora ya Maji,kama hawapati kuna mradi gani ninaoutekeleza na hakuna mradi mpango gani upo?.
Mhandisi Sanga

Pia amewataka kusimamia miradi ya Maji inayongwa na kuhakikisha inajengwa kwa ubora na kwa thamani ya fedha inayotumuka katika mradi husika.

"Miradi msingi hivi sasa tunaitekeleza kwa fefja za" force account" sasa kama mradi unapaswa kukaa miaka 50 na iwe hivyo siyo mradi unajengwa kwa kutumiabfefha nyingi halafu baada ya muda kidogo unakuwa na nyufa,hii siyo sawa"amesema Katibu Mkuu huyo

Awali akiongea kabla ya kuongea mgeni rasmi Katibu Mkuu Utumishi Dkt Francis Michael amesema watumishi wa Umma nchini hawana budi kuzingatia maadili ya utumishi Wa Umma na kuepuka mihemuko ya Kisiasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 mwaka huu.
 Tunaelekea kwenye kipindi Cha Uchaguzi lazima tujue majukumu yetu nini sisi Kama watumishi wa umma hilo lazima kila mtumishi kulitambua bila kusahau uwadilifu.
Dkt Francis Michael

Amesema kwenye utumishi wa Umma Kuna sheria na kanuni zinazomkataza mtumishi huyo kufanya ikiwemo kutumia nafasi zao kwa manufaa yao au kupendeea mtu fulani.

Pia mtumishi anatakiwa kulinda ubadhilifu au upotevu wa fedha ni wajibu wenu kusimamia fedha kwa manufaa ya Tasisi na Serikali kwa ujumla.

 SIASA

Aidha amesema katika suala zima la siasa watumishi wa Umma wanahaki ya kidemokrasia kuchagua na kuchaguliwa au kuwa mwanacha wa Chama fulani Cha siasa nchini.

Pia amesema mtumishi wa umma kushiriki katika masuala ya siasa katika vyama vyao inaruhudiwa ila tu wasipendelee mtu kwakuwa mtumishi huyo au watumishi hao watakuwa na mapenzi na Chama fulani Cha siasa .

Mtumishi wa Umma huzuiliwi kujihusisaha na siasa ila mnatakuwa kuzingatia yafuatayo ambayo pahala na sehemu yoyote ya kazi mtumishi kuingiza siasa
Dkt Francis

Na kuongeza kusema kuwa"Sio tu kuoeleka siasa mahala pa kazi Bali hata kuvaa nguo zenyenembo ya Chama fulani kazini hairuhusiwi Wala kutumia gari ya Serikali kufanya kampeni," amesema Katibu Mkuu huyo.

Amesema utakuta mtumishi kwasababu tu anamapenzi na Chama fulani Cha siasa basi anakuwa anatoa  taarifa au nyaraka za Serikali na kupeleka katika Chama fulani Cha siasa huko ni kutoa Siri za Serikali.

" Katika masuala ya siasa mtumishi wa Umma hanabudi kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa za utumishi wa Umma na utawala bora," amesema Dkt Farancis.

Naye Naibu Mwanasheria Mkuu Serikali ,(DAG) Dkt. Evaristo Longopa, amesema kila mtu anahaki kikatiba kuchagua na kuchaguliwa na kutoa maoni yao.

Hata hivyo amesema katika ibara ya 20 kwenye katiba yetu inasema raia yoyote anahaki ya kushiriki na wenzake kwenye vikundi vya ushirika au vyama vya siasa.

Amesema ibara ya113 (a) inakataza majaji na mahakimu kujiunga na Chama chochote Cha siasa kwa sababu wenywe ndio watoa haki hivyo hawatakiwi kuwa  wanachama wa Chama Cha siasa.


Post a Comment

0 Comments