WAZIRI SIMBACHAWENE AHOJI MCHAKAO MREFU WA KUPATA PASPOTI



 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George  Simbachawene leo ametembelea
viwanja vya Nane Nane Kanda ya Kati yanayoendelea jijini Dodoma

📌NA HAMIDA RAMADHANI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George  Simbachawene, amesema kuwa watanznia wengi  wanashindwa  kupata paspoti za kusafiria kutokana na mchakato wa upatikanaji wake kuchukua muda mrefu.
Aidha ameitaka idara ya uhamiaji kutofanya urasimu wakati wa utoaji wa paspoti za kusafiria.
Simbachawene ametoa kauli hiyo leo August 7 mwaka huu  wakati alipokuwa akikagua mabanda ya maonesho ya wakulima nane nane yanayofanyika katika viwanja vya nanenane Nzuguni Jijini hapa.
Akizungumza na maofisa uhamiaji katika banda lao la maonesho Waziri huyo amesema  ni haki ya kila mtanzania kuwa na paspoti ya kusafiria lakini hawapati kutokana na mlolongo kuwa mkubwa
Amesema wapo watanzania wengi ambao wanatakiwa kuwa na paspoti za kusafiria lakini wanashindwa kupata kutokana na urasimu uliopo kwa kupewa mlolongo mkubwa jambo ambalo linakatisha tamaa.
Sasa napenda kusema kuwa ni vyema mkatoa elimu kwa watanzania ili waweze kupata pasport zao za kusafiria kwani ni haki yao ya kuwa na pasi ya kusafiria
Simbachawene.
Waziri Simbachawene akiangalia moja ya bidhaa ndani ya mabanda katika uwanja
wa maonesho ya Nane Nane Katika ya Kati yanayoendelea jijini Dodoma.

Kwa upande wake Afisa uhamiaji Mkoa wa Dodoma,Ramadhani Makala amesema kwamba licha ya kila mtanzania kuwa na haki ya kupata paspoti ya kusafiria lakini mwombaji lazina akidhi vigezo.
Amevitaja vigezo hivyo na kuvieleza kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na cheti cha kuzaliwa au cha mzazi wake,namba ya utambulisho ya NIDA au kiapo cha mahakama au mwanasheria.
Pia amesema kuwa kwa sasa fomu za kuomba pasporti ya kusafiria zinapatikana kwa njia ya mtandao ambayo unaweza kuijaza na kuambatanisha vitu muhimu vinavyotakiwa.

Post a Comment

0 Comments