WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA NA MPANGO WA KITAIFA WA MIAKA 10 KATIKA VIWANDA




📌NA HAMIDA RAMADHANI
IMEELEZWA kuwa Kaizen ni falsafa ya uongezaji endelevu wa ubora na tija kwa njia ya kushirikisha watumishi na uongozi katika kampuni husika ambayo hutumika kama zana ya kujikagua kuhusiana na uongezaji endelevu wa tija na ubora kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika uwajibikaji na katika kuhimili ushindani.

Kutokana na hayo Wizara ya Viwanda na Biashara imeandaa Mpango wa Kitaifa wa miaka kumi wa uongezaji endelevu wa ubora na tija katika sekta ya uzalishaji viwandani 2020-2030 kupitia mradi wa falsafa ya Kaizen .

Akizindua mpango huo jana jijini hapa ,Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Riziki Shemdoe alisema kama falsafa ya Kaizen mradi ambao unafadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia shirika lake JICA ,ikitumika vizuri nchi inaweza kufikia uchumi wa kati wa juu ifikapo mwaka 2025.
“Julai mosi mwaka huu Benki ya Dunia iliitangaza Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kipato cha kati ,kimsingi tumewahi kufika hapo kabla ya wakati tuliokuwa tumejipangia, maana malengo ya kufikia hatua hiyo ilikuwa ni mwaka 2025 ,hii inamaanisha tumefanya kazi ya ziada na kufikia lengo kabla ya muda,
“Changamoto ni kuendelea kuidumisha hatua hiyo ya uchumi wa kati ,lakini kama mnavyofahamu tupo katika uchumi wa kati wa chini ,sasa tunapaswa kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 tuwe tumefikia uchumi wa kati wa juu ,na hili sasa liwe ndio lengo letu na kupitia Kaizen nina uhakika kama tunaweza kuitumia falsafa hii vizuri tunaweza kufikia hapo.”amesisitiza Katibu Mkuu huyo
Kwa mujibu wa Profesa Shemdoe ,uchumi wa nchi utaweza kwenda mbele na kwa haraka zaidi itakapokuwa  na uwezo wa kuzaisha bidhaa za kupeleka kwenye viwanda vyake .
“Sisi wote hapa tunajishughulisha na viwanda kwa namna moja ama nyingine,uchumi wa nchi utaweza kwenda mbele pale tu tunapokuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa za kupeleka kwenye viwanda vyetu ,hapa sasa tujadili namna ambavyo tunaweza kutoka hapa tulipo ili tuweze kufika uchumi wa kati wa juu”Profesa amesema.
Aidha alisema,katika mwaka 2019/2020 wizara ilifanya tathimini ya hali ya utekelezaji wa miradi ya Kaizen ambapo pamoja na mambo mengine tathimini hiyo ilibaini ongezko la ubora na tija kwa bidhaa za viwandani huku akisema hatua hiyo imesababishwa  na usimamizi bora wa rasilimali watu,muda na miundombinu
Amesema katika tathimini hiyo ilionekaa kwamba, kwenye utekelezaji wa mafunzo yaliyofanywa kwenye viwanda wameweza kuokoa shilingi  300 milioni ambazo zingeweza kutumika ndivyo sivyo lakini kwa kutumia falsafa hiyo  fedha hiyo imeweza kuokolewa.
Aidha amesema kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa mradi huo ,yameipatia fursa Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano Kaizen Barani Afrika Juni 2021 yatakayohusisha nchi 16.
Hii itakuwa ni fursa ya kuvutia wawekezaji lakini pia ni fursa ya kutangaza vivutio vya utalii nchini na hatimaye kuchangia uchumi wan chi,hivyo ninaomba kuchukua fusa hii  kuutangazia umma wa watanzania kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa kongamano  la Kaizen barani Afrika litakalofanyika Juni 2021, tunatakiwa kujiandaa mapema ili kunufaika na fursa kupitia kongamano hilo.
Profesa Shemdoe
Pia Tanzania kupitia viwanda vyake vya A-Z ,mwaka jana ilishinda tuzo ya Afrika katika utekelezaji  wa mradi wa Kaizen.
Awali Mkurugenzi Idara ya Viwanda Mhandisi Ramson Mwilangali amesema,hiyo ni  mara ya kwanza kwa maadhimsho hayo kufanyika nchini huku akisema ni matumaini yake kuwa yatakuwa endelevu .
Amesema lengo la maadhimisho hayo  ni kutoa fursa kwa washiriki na jamii kwa ujumla kuielewa falsafa hiyo na kukuza uchumi nchini.





Post a Comment

0 Comments