BENKI YA WATU WA ZANZIBAR NA BENKI YA POSTA KUBORESHA HUDUMA KWA WOTE



📌NA SAIDA ISSA

BENKI ya watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kushirikiana na Shirika la Posta Tanzania imejidhatiti kutoa huduma kwa wahitaji na wananchi ambao wamekuwa wakienda masafa marefu kutafuta huduma.

Aidha uongozi wa Benki hiyo umeadhimia kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wote wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Seif Suleiman Mohammed meneja wa tawi la PBZ Dar es salaam pia ni msimaizi wa mafunzo ya huduma za benki kwa mawakala wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na adhima ya benki hiyo katika kuimarisha huduma zake.

Aidha amefafanua kuwa katika kuhakikisha huduma za kibenki zinaimarishwa kwa wananchi wote hapa nchini wamenza kutoa mafunzo ya namna benki ya watu wa zanIbar wanavyofanya kazi.

Mafunzo haya yanatolewa hapa Dodoma kwa maafisa mbalimbali kutoka kwa mikoa tofauti ili kuweza kuboresha utoaji wa huduma za benki hiyo kwa wananchi.
Seif Suleiman Mohammed

Amesema kuwa hii ni kutikana na kwamba Dodoma ni Mkao makuu na pia ni katikati ya Nchi hivyo benki ya watu wa zanzibar imedhamiria kutoa huduma.

Wananchi wamekuwa wakienda katika masafa marefu ili kutafuta huduma nakuwafanya wapoteze muda mwingi na gharama.

Kwa upende wake Rehema Mbunda  meneja  wa huduma za fedha na uwakala shirika la posta makao makuu Dar es salaam alisema kuwa Benki ya watu wa Zanzibar imeamua kuingia ubia na shirika la posta Tanzania kwa sababu tayari kwa bara kuna matawi 360 na wanatoa huduma hivyo wananchi wengi zaidi watanufaika na ubia huo.

Wananchi watarajie kupata huduma nzuri sababu posta imetapakaa katika sehemu nyingi na sasa benki ya watu wa zanzibar imejidhatiti kuwafata wananchi mpaka vijijini ili kuwapatia huduma.
Rehema Mbunda.

Amesema kuwa Benki ya watu wa Zanzibar imeona ni bora ikatoa mafunzo kwa Maafisa kutoka mikoa tofauti tofauti  ili kuweza kutoa huduma za kibenki kwa wananchi.


Post a Comment

0 Comments