CDF YATOA MAFUNZO YA UONGOZI NA STADI ZA MAISHA KWA WANAFUNZI



📌NA HAMIDA RAMADHANI

SHIRIKA la Jukwaa la Utu wa Mtoto (Children’s Dignity Forum-CDF) linalotekeleza Mradi wa Haki ya Binti awamu ya Pili Wilayani Mpwapwa limefanya mafunzo ya uongozi na Stadi za Maisha kwa wanafunzi wilayani humo lengo likiwa ni kuwasaidia wanafunzi hao kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.

Akizungumza na CPC Blog mara baada ya kumalizika kwa Mafunzo hayo Meneja utekelezaji wa Miradi ya CDF Bwana Evance Rwamuhuru amesema mafunzo hayo yamelenga mambo makubwa manne ambayo ni kujitambua katika malengo waliojiwekea ,kuwajenga katika stadi za maisha,kuwajengea uwelewa katika masuala ya afya ya uzazi na kuwajengea uwezo katika masuala ya uogozi.



Mafunzo haya yamelenga kuwajenga wasichana pamoja na wavulana wa shule za msingi na sekondari ambao wako ishirini na mbili tumewafundisha wao kama waelimisha rika kwa maana ya kwamba wao wajifunze na waende kuwafundisha wenzao katika jamii walizotoka
Evance Rwamuhuru


Wanafunzi waliopata mafunzo hayo ni kutoka shule za Sekondari Pwaga,Kibakwe,kimagai huku kwa upande wa shule za Msingi zikiwa ni Lupeta pamoja Ibumila.

Kupitia mafunzo haya wanaweza kujiweka malengo ya sasa na ya baadae wanapita katika mchakato mzima wa kujua kuwa wao ni wakina nani ,wana ndoto gani za maisha lakini changamoto gani wanaweza kukabiliana nazo lakini sasa wanawezaje kuzikabili hizo changamoto.Evance Rwamuhuru

Amesema matarajio ya mradi huo ni kuhakikisha kwamba watoto wa kike wanafahamu haki zao na waweze kujisimamia sawa sawa kwani hawatarajii kuona watoto wa kike wanashindwa kulendelea na masomo yao kwasababu ya kupata ujauzito.

Lidya Joseph Joseph ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Pwaga amesemaa amejifunza namna ya kujitambua katika mafunzo hayo kujua mwanafuni shuleni amekwenda kufanya nini .

''Nimejifunza namna ya kuweka malengo katika  masomo yangu, lakini kitu kingine nimejifunza juu ya hedhi salama, hivyo unapokuwa katika hedhi ni vitu gani msichana ufanye unapokuwa katika hedhi ikiwemo pia kutojichafua kwani hedhi sio ugonjwa lakini pia tumejifunza stadi za maisha hii itanisaidia sana katika masomo yangu na hata katika maisha kwani inatusaidia namna ya kutatua matatizo ambayo yako, nimejifunza  pia namna ya kujiwekea malengo kwa miaka mitano,kumi,kumi na tano na kuendelea'' Lidya

Wanafunzi wakijadiliana jambo katika Mafunzo ya Uongozi na Stadi za Maisha

Kwa upande wa Jonh Dominick mwanafunzi wa shule ya sekondari pwaga kidato cha tatu amesema yeye ni kwa namna gani wavulana wanapaswa kuwasaidia watoto wa kike pindi wanapokuwa katika kipindi cha hedhi wakiwa shuleni na sio kuwacheka.

Jumla ya wanafunzi 22 wamehudhuria katika Mafunzo ya uongozi na Stadi za Maisha kwa wanafunzi wilayani Mpwapwa wakiwa na walimu walezi wao 5.

Mafunzo hayo yamefanywa na Shirika la Jukwa la Utu wa Mtoto (Children's Dignity Forum CDF) Wilayani Mpwampwa  chini ya Mradi wa Haki ya Binti awamu ya Pili kwa Ufadhili wa Comic Relief.

Post a Comment

0 Comments