DIWANI KILIMANI 'AWASHA MOTO',AJIVUNIA MAFANIKIO YAKE KUOMBA KURA OKTOBA 28





📌NA BARNABAS KISENGI

Mgombea Udiwani  wa Kata ya Kilimani jijini Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Neema Mwaluko amezindua kampeni ya uchaguzi katika kata hiyo tayari kwa mapambano ya kutetea nafasi yake.

Awali akizungumza katika mkutano wa uzinduzi huo uliofanyika katika mtaa wa Chinyoya Neema amesema katika miaka mitano iliyopita katika baadhi ya maeneo katika kata hiyo kulikuwa na changamoto kubwa mbili zikiwemo miundombinu ya barabara na urasimishaji wa  viwanja vya makazi  kwa wananchi wa maeneo hayo.

Ninashukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwezesha  kufanikisha jambo hili pia kipekee niwashukuru mbuge Anthony Mavunde na mwenyekiti wa mtaa wa chinyoyo Faustina Bendera kwa ushirikiano wao hadi sasa tumefanikisha wananchi wetu wamerasimishiwa ardhi kwa kupimiwa.
Neema Mwaluko

Aidha Neema amesema akipewa ridhaa tena ya kuongoza miaka mitano  vipaumbele vyake ni kuhakikisha anatengeneza miundombinu ya barabara ujenzi wa shule  ya msingi ya kata,zahanati na soko ili wananchi wa kata ya kilimani wapate huduma

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde amesema ili maendeleo yakamilike katika kata ya Kilimani amewaomba wananchi wachague mafiga matatu ya CCM,yaani Rais, Mbunge na Diwani Neema Mwaluko ili washirikiane kuleta maendeleo.


Katika uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM wa Wilaya Dodoma Mjini,madiwani wateule na mbunge viti maalumu Mariam Ditopile ambaye aliwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ifikapo October 28 mwaka huu ili wapige kura na kukipatia Chama Cha Mapinduzi ushindi wa kishindo.


Post a Comment

0 Comments