JAMII YASHAURIWA KUTUMIA DAWA ZA TIBA ASILI



📌NA HAMIDA RAMADHANI

JAMII imeshauriwa kuondoa mtazamo hasi kuhusu dawa za tiba asili na badala yake imetakiwa kutumia dawa hizo kwani ni dawa zitokanazo na mimea kwani nibora kwa matumizi ya binadamu .

Akizungumza na waandishi wa habari  katika viwanja  vya Nyerere Square Mkurugenzi kutoka Khaira Herbal Clinic  Dkt. Sungura Rashid Sungura  kutoka  mkoani Kigoma kwenye Maadhimisho ya siku ya tiba asili ya mwafrika amesema dawa hizo ni dawa zitokanazo na miti iliyopo nchini na inapimwa na mkemia Mkuu kwa matumizi sahihi ya binadamu.

 Zamani hapakuwa na hospital  nyingi wazee wetu walitumia dawa za asili na ndio maana kama ukifatilia utasikia kuna yale maneno huo udongo wa zamani yani na wana nguvu kabisa na waliishi kwa kutumia dawa hizi za asili
Dkt. Sungura

Aidha amesema  kufuatia janga la ugonjwa wa Corona  dawa za tiba asili zimesaidia kutokomeza ugonjwa huo hapa nchini na kumpogeza Rais Magufuli kwa kuruhusu wao kama waganga wa tiba asili watafute dawa.

"Tunaona nchi zingine kwa sasa wanajiuliza Corona imeishaje nchini Tanzania na niseme tu majuzi nilikutana na gari imejaza malimao inapeleka nje ya nchi siwezi taja nchi gani  karibia magunia 200 lakini wao wanashangaa na kujiuliza Corona imeishaje nchini Tanzania kwasababu wanataka kujaribu dawa zetu zilizosaidia kumaliza ugonjwa wa Corona,"amesema Dkt Sungura

Mimi elimu hii ya kutibu nilifundishwa na mama mkwe wangu basi nami nikawa najiendeleza yani kama wanavyofanya mikutano wenzetu wa hospital na sisi hivyo hivyo nikawa nikikutana na waganga wenzangu tunaelekezena dawa hizi zinatibu nini.
Dkt. Sungura

"Nyie wenyewe mashahidi waandishi  wa Habari juzi hapa mlikuja mkaona kuna mtu anatoa shuhuda alikua anasumbuliwa na uric acid akatumia dawa zangu kwahiyo niseme dawa hizi zinafanya kazi vizuri  na mtu anapotumia dawa hizi analeta majibu kwa haraka na sisi huwa tunaweka mawasiliano mtu anakupigia anakupa mrejesho " amesema Dkt Sungura



Sambamba na hayo Sungura ameishukuru serikali kwa kuwaasa wao  kama waganga watenge misitu yao kwaajili ya kuchimba dawa ili wasiharibu uoto wa asili.

Hata hivyo maadhimisho ya siku ya Tiba asili ya Mwafrika yalianza rasmi mwaka 2003 baada ya Mawaziri wa afya wa nchi wanachama wa shirika la afya Duniani Kanda ya afrika kuridhia kuwepo kwa kwa sherehe hizo.


Post a Comment

0 Comments