📌BBC SWAHILI
KASKAZINI mwa
Msumbiji, mapigano yanaendelea na kuongezeka hali ambayo imelazimisha maelfu ya
watu kutoroka makazi yao.
Sasa hivi idadi kubwa
ya raia hao wanakimbilia nchi jirani ya Tanzania kulingana na mkurugenzi wa
Shirika la Chakula Duniani eneo la Kusini mwa Afrika alipozungumza na BBC.
Makadirio kutoka
Shirika la Umoja wa Mataifa na wadau wengine ni kwamba idadi ya kundi hilo la
wakimbizi ni karibu watu 1000.
Aidha kulingana na
Shirika la Chakula Duniani, sasa hivi serikali ya Tanzania ndio inayosimamia
mahitaji ya kundi la wakimbizi walioingia nchini humo kutoka Msumbiji hivi
majuzi.
Pia kuna taarifa
kwamba unyanyasaji wa haki za binadamu katika eneo la Cabo Delgado umekuwa
ukiongezeka huku mapigano kati ya wanamgambo wa Kiislamu na vikosi vya serikali
yakiendelea.
Mpaka kati ya Msumbiji
na Tanzania ni mto Ruvuma, na eneo la pwani ya bahari. Katika kipindi cha miaka
mitatu iliyopita, Msumbiji imeshuhudiwa idadi kubwa ya watu wakilazimika
kutoroka makazi yao hasa katika mkoa wa Cabo Delgado huku wengine wakielekea
eneo la kusini la Nampula, amesema mkurugenzi wa WFP.
Kulingana na Lola
Castro mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani eneo la Kusini mwa Afrika, wiki
kadhaa zilizopita Shirika hilo lilipata taarifa kwamba kulikuwa na kundi la
watu lililovuka mpaka kutoka mto Ruvuma na kuingia eneo la Mtwara nchini Tanzania.
Inasemekana kwamba
baadhi ya watu walitumia boti huku wengine wakiogolea katika mto Ruvuma kuingia
nchini Tanzania.
Usafiri ulizoeleka katika mto Ruvuma ni mtumbwi pia wanavuka kwa kutumia boti hadi visiwani eneo la delta la Msumbiji na Tanzania
Lola Castro.
Hatahivyo, tatizo ni
kwamba wakimbizi katika eneo la Cabo Delgado na Nampula ambapo kulikuwa na watu
karibu elfu 310, idadi hiyo imeongezeka pakubwa katika kipindi cha mwezi mmoja
uliopita.
''Hii imesababishwa na
ukosefu wa usalama na mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea. Raia wanatoroka
makwao na kuacha kila kitu nyuma, na kinachotatiza zaidi ni kwamba wamekuwa
wakiondoka tangu mwezi uliopita, kilele cha msimu wa mavuno
''Na kundi hilo halina
chakula wakati ambapo shirika la chakula duniani limekuwa likiwapa chakula kwa
karibu mwaka mmoja sasa hadi watakapoweza kurejea kwenye makazi yao na
kurejelea shughuli za kilimo,'' amesema Lola Castro.
Shirika la Chakula
Duniani limasema raia wa kaskazini mwa Msumbiji wamekuwa wakishuhudia ukosefu wa
usalama na mapigano yamekuwa yakiendelea kwa karibu miaka mitatu, raia
wameuawa, wametoroka makazi yao na sasa hivi wanakimbilia Tanzania na kuna
uwezekano hali ikaendelea kuwa mbaya zaidi pengine wafanikiwe kurejea nyumbani,
lakini tayari hali inatarajiwa kuwa mbaya kwa mwaka mmoja kwasababu msimu
mwingine wa mavuno unatarajiwa kuwa miezi ya Machi, Aprili na Mei mwaka ujao
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
0 Comments