📌NA DOTTO KWILASA
TUME ya Taifa ya uchaguzi (NEC)imeandaa daftari la huduma ya
wapiga kura lenye wapiga kura wapatao 29,188,347 na vituo vya kupigia kura
vipatavyo 80,155.
Mkurugenzi wa Tume
hiyo Dk.Wilson Charles Mahera alisema hayo wakati akitoa taarifa kwa umma juu
ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Amesema kwa sasa tume hiyo inashughulika na kuratibu kampeni za uchaguzi kwa na
manunuzi na usambazaji wa vifaa vya
kupigia kura katika majimbo mbalimbali nchini .
Licha ya hayo Mkurugenzi huyo amesema tume hiyo imeelekeza
nguvu katika kutoa elimu ya mpiga kura ikiwa ni pamoja na kuandaa maandalizi ya
kuwateua wasimamizi wa vituo vya kupigia kura.
Katika hatua nyingine Tume hiyo imekanusha taarifa
zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii zikimtuhumu Rais John Magufuli kufanya kikao na
Wakurugenzi na wasimamizi wa uchaguzi mjini Dodoma.
Amefafanua tuhuma hizo,Dk.Mahera amesema taarifa hizo ni za
uongo ,uzushi na zenye kuleta taharuki miongoni mwa watanzania na wapiga kura
na kujenga picha kuwa uchaguzi mkuu hautakuwa huru na haki na kwamba hata
wakishindwa kihalali basi watataka watanzania wawaunge mkono kuvuruga amani kwa
ajenda zao binafsi.
“Tangu tarehe 25.09.2020 na 26.09.2020 tunaendelea na ziara
ya kukagua na kuratibu maandalizi ya uchaguzi katika majimbo ya mikoa ya
manyara ,Arusha na Kilimanjaro na mikoa mingine na kote nilikopita nimekutana
na wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo yao ya kazi,
Na katika hili niudhihirishie Umma wa watanzania kuwa taarifa zilizotolewa na Tundu Lissu zinalenga kuvuruga amani jambo ambalo halikubaliki hivyo kwa mamlaka ya kisheria niliyonayo ya Tume ya uchaguzi tayari nimemwandikia Lissu barua ya kumwita katika kamati ya kikao cha maadili cha kitaifa aje kujielezakwa Ushahidi
Dk.Mahera.
Pamoja na hayo NEC inawataka wagombea wa vyama vyote kufuata
sheria ,kanuni na taratibu za nchi ili kulinda amani katika kipindi cha kampeni
za uchaguzi kilichobaki kwa kujali muda wa kampeni ,ratiba na kuepuka matusi
,tuhuma zisizo na Ushahidi zenye lengo la kuwadanganya watanzania kuwapa kura
za huruma.
0 Comments