WATOTO 8 WANA SIKOSELI KWA KILA WATOTO 100 WANAOZALIWA

Kaimu Mkurugenzi wa Tiba,Wizara ya afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,
Wazee na watoto Sarah Maongezi


📌NA DOTTO KWILASA

JUMLA ya watu 1000 huzaliwa na ugonjwa wa Sikoseli kila siku duniani huku nchini Tanzania watu  11 Elfu wanakadiriwa kuzaliwa na ugonjwa huo kila mwaka.

Hayo yameelezwa jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba,Wizara ya afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia ,Wazee na watoto Sarah Maongezi wakati akizindua mwezi wa kuelimisha jamii juu ya ugonjwa wa Sikoseli .

Aidha maadhimisho hayo ambayo huanza kila mwaka  ifikapo Septemba 1 hadi 9 yana lengo la kupeana uelewa wa Sikoseli kati ya wadau wa afya na jamii kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Tanzania ni nchi ya tano duniani kuwa na idadi ya wagonjwa wengi wa Sikoseli huku ikishika nafasi ya nne barani Afrika.

Nchi zenye wangonjwa wengi duniani ni Nigeria,India,Kongo,Angola na Tanzania,ambapo kwa Afrika Tanzania inashika nafasi ya nne hali inayopaswa kutiliwa mkazo zaidi kuhakikisha ugonjwa huu unazuiwa.
Sarah Maongezi

Licha ya hayo alisema ,nchini Tanzania ,kila watoto 100 wanaozaliwa nchini ,8 kati yao wana ugonjwa wa Sikoseli.

Ameongeza kuwa,licha ya juhudi nyingi zinazofanywa na wizara ya Afya katika kuelekeza nguvu za uelimishaji jamii juu ya ugonjwa huo ,jamii bado haina uelewa wa kutosha hali inayosababisha unyanyapaa kwa waathirika wa ugonjwa huo.

Kutokana na hayo daktari bingwa wa magonjwa ya damu kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa Stella Malangahe alisema ugonjwa huo husababisha athari mbalimbali ikiwemo ini,figo,mapafu,kupooza na hata vifo vya mapema.

Amesema kuwa mtu mwenye ugonjwa wa selimundo huongezewa damu marakwa mara kwasababu chembechembe zao haziwezi kukaa muda mrefu.

Kukiwa na mgonjwa wa Sikoseli basi lazima mama au baba yake ana ugonjwa huo.
Stella Malangahe
 
Daktari bingwa wa magonjwa ya damu kutoka
Hospitali ya Benjamini Mkapa Stella Malangahe


Akizungumzia dalili za ugonjwa huo Dr.Malangahe amesema kuwa ni pamoja na maumivu ya mara kwa mara yanayojirudia, kuvimba miguu,mikono na hasa mtoto anapokuwa ametimiza miezi 6,kulia Sana na kupata manjano mikononi na miguuni,kupungukiwa damu mara kwa Mara.

Licha ya ugonjwa huo kuonekana ni tishio,Dr.Malangahe amesema kwa sasa unatibika na kwamba mgonjwa anatakiwa kuwekewa uboho wa ndugu wa karibu ambaye hana historia ya ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Sikoseli unazuilika ,nawashauri wenza kabla ya kuingia kwenye mahusiano wanapaswa kufanya vipomo vya kubaini vinasaba vya ugonjwa huo ili kuzuia kupata watoto wenye Sikoseli.
Stella Malangahe

Post a Comment

0 Comments