NEC YAWAONA WENYE ULEMAVU,YAWATENGEA VIFAA MAALUMU VYA KUPIGIA KURA

 


📌NA DOTTO KWILASA.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC ) imewatoa hofu wapiga kura  wenye mahitaji maalumu kuwa maelekezo yametolewa kwa watendaji wa uchaguzi kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu,wajawazito,akina mama wanaonyonyesha waliokwenda na watoto vituoni,wazee na pamoja na wagonjwa.

Wito huo umetolewa jana jijini hapa na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji Mstaafu Mbarouk S.Mbarouk wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Dodoma ambao umehusisha viongozi wa dini,wawakilishi wa vijana , wanawake,wenye ulemavu na wazee wa kimila.

Akitoa ufafanuzi ,Makamu mwenyekiti huyo ameeleza kuwa, kwa watu wenye ulemavu wa kuona ,kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na kifaa cha maandishi ya nukta nundu (Tictile Ballot Folder) hiyo ni kwa wale wanafahamu kutumia maandishi hayo na kwa wasioweza wataruhusiwa kwenda kituoni na mtu anayemwamini wakuweza kumsaidia.

Kwa mujibu wa Jaji Mstaafu huyo amesema hatua imefikiwa baada ya Tume kupata idadi ya watu wenye ulemavu waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu ambapo kuna jumla ya watu 13,211 wenye ulemavu na kati yao wenye ulemavu wa macho ni 2223,4911 wana ulemavu wa mikono na 6077 wana ulemavu wa aina nyingine.

Wenye ulemavu wa kuona kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na kifaa cha maandishi ya nukta nundu  hiyo ni kwa wale wanafahamu kutumia maandishi hayo na kwa wasioweza wataruhusiwa kwenda kituoni na mtu anayemwamini wakuweza kumsaidia

Jaji Mstaafu Mbarouk S.Mbarouk

Hata hivyo, Jaji Mbarouk amesema kwa wenye ulemavu wa viungo vituturi (viboksi vya kupigia kura) vitakavyotumika kupigia kura vinaruhusu kuwahudumia kwani kuna pande mbili tofauti ambapo upande mmoja kuna urefu wa kutosha na kikigeuzwa kinakuwa kifupi kumuwezesha mwenye ulemavu wa viungo kupiga kura.

Katika hatua nyingine NEC imevitaka Vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Urais,Ubunge na Udiwani kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kipindi cha kampeni zao ikiwa ni pamoja na  kuepuka lugha za kashfa ,maneno ya uchochezi ambayo yatatishia amani ya nchi.

Makamu mwenyekiti huyo  amesema,ikiwa maadili yatazingatiwa itasaidia kuepusha malalamiko kwa jamii na kwamba haki itasaidia kuiweka Tanzania salama kimataifa na kuchochea uchumi.

Kama kutakuwa na malalamiko yoyote basi hatua stahiki zichukuliwe ikwemo kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili ndani ya muda uliowekwa na si vinginevyo.

Jaji Mstaafu Mbarouk S.Mbarouk

Aidha amesema Tume inaendelea kusimamia na kuendesha uchaguzi kwa kutumia sheria za uchaguzi hivyo vyama vya siasa,wagombe na wananchi wanakumbushwa kuwa  katika kipindi hiki sheria nyingine za nchi hazijasimama  hivyo wanapaswa kujihadhari na vitendo ama matamshi ambayo kusababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi.

‘’Tume inawahakikishia wananchi kuwa imejipanga katika kusimamia uchaguzi wa mwaka huu kwa kufuata katiba sheria,kanuni na miongozo mbalimbali na kuwa kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kufuata taratibu watanzania wataweza kupiga kura kwa amani siku ya uchaguzi’’anasema

Makamu Mwenyekiti wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Mbarouk  S.Mbarouk,akiwa katika picha za pamoja  na baadhi ya Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.


 


Post a Comment

0 Comments