OSSIEC YATOA MSAADA KWA MAMA ALIYETELEKEZWA NA MUME,KISA MTOTO MWENYE UALIBINO

 


📌NA HAMIDA RAMADHANI

TAASISI isiyo ya kiserikali  ya Organisation  for Social  Support Initiative  and Environment  Conservation  (OSSIEC)  imetoa  msaada wa chakula na mtaji  wa biashara  kwa mama Sara Ulanga  mwenye mtoto albino  anayeishi katika kata ya Chang'ombe alietelekezwa na mzazi mwenzie mara baada ya kujifungua mtoto mwenye ualbino. 

Akizungumza na Waandishi wa habari leo  mara baada  ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi kutoka OSSIEC Kennedy Kasian  amesema  wao kama taasisi wameguswa kumtembelea na kutoa msaada  kwa mama  huyo  baada ya kupewa taarifa  ya mazingira anayoishi mama  huyo na mtoto.

Hii ni mara ya pili, tulikuja awali na ni kweli  tumeona mama huyu anapitia wakati mgumu hasa katika suala zima la kumhudumia mtoto katika afya, chakula  mavazi na malazi ndipo  tukaona kuna jambo tunaweza kufanya kwa mama huyu ndio maana leo tupo hapa"amesema Kasian

Watu wenye ualibino mara nyingi hufariki  kwa  saratani ya ngozi  hivyo  inahitajika juhudi kubwa kuhakikisha wanapatiwa  kofia, mafuta, nguo, miwani na chakula.

Kennedy Kassian

 

Aidha ametoa wito kwa jamii kuacha  kuwatenga wazazi na watoto wenye ualibino  kwani wanaume wengi wamekuwa wakiwakimbia watoto  wenye ualibino  huku wakiwaita kuwa ni watoto wa laana. 

Sambamba na hayo Mkurugenzi Kassian ametoa rai kwa asasi zote za kiraia kuendelea kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu. 

Hata hivyo ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kupigana  na kuhakikisha maisha ya watu wenye ualibino yanakuwa salama. 

Sasa  hivi ni kipindi cha uchaguzi lakini hali ni shwari hatujasikia wala kuona matukio  yoyote  yanayowahusu ndugu zetu albino hii yote ni  jitihada  ya serikali kuhakikisha wanaweka salama maisha ya watu wenye ualbino.Kennedy Kassian

Naye afisa utawala kutoka OSSIEC  Farida Msuya amesema ulemavu siyo ugonjwa na wala hauambukizi hivyo watu wenye ualbino wanatakiwa kulindwa na kupendwa kama watu wengine. 

Kwa upande  wake mama mwenye mtoto huyo Sara Ulanga ameishukuru taasisi ya OSSIEC kwa msaada huo kwani  maisha yake ni magumu na yakubahatisha hasa katika zoezi la  kumlea mtoto huyo. 

Mimi baada ya kujifungua  mtoto huyu nilitengwa na kila mtu  marafiki zangu,   ndugu,na hata mzazi mwenzangu niliezaa nae  alinikimbia  mpaka aliwahi  kudiliki  kusema nimtupe mtoto huyu chooni  kwa maana hana uhakika kama mtoto huyo ni damu yake kwakua  hakuwahi kufikiria kama atapata mtoto mwenye ualibino

Sara Ulanga

 Sara ametoa wito kwa  jamii na wazazi  wenye watoto wenye ualbino  kuwapenda Kwani  ni watoto kama walivyo  watoto wengine

OSSIEC   ni shirika  lisilo la kiserikali liloanzishwa  june  2020  ikiwa imejikita kwenye Elimu, afya, Mazingira, na kusaidia watu wenye mazingira magumu. 

Post a Comment

0 Comments