📌NA DOTTO KWILASA
SERIKALI imesema ipo kwenye mchakato wa kuongeza
uzalishaji wa mafuta ya kula nchini kwa
mazao yote yanayotoa mafuta ikiwemo
alizeti, na michikichi ili kuzuia
kuingia kwa mafuta kutoka nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa
jijini hapa na Mkurugenzi wa udhibiti ubora {TBS} Lazaro Msasalaga wakati akitoa mafunzo kwenye semina
kwa wazalishaji,wasambazaji,na wauzaji wa mafuta ya kula.
Amesema lengo kubwa la serikali ni kuzingatia mahitaji makubwa ambayo kwa
sasa wananchi wanahitaji ili kuweza
kuzalisha mafuta ya kula kwa wingi nchini.
Waziri ana mradi mkubwa wa kupanda michikichi kule Kigoma lengo kubwa ni kuongeza uzalishaji wa mafuta nchini, na si kwenye michikichi tu inaenda kuangalia na uzalishaji wa mazao mengine kama alizeti na namna Mkoa husika unavyoweza kuzalisha zao hilo
Aidha amesema
katika mafunzo hayo wamepita
wilaya zote za mkoa wa Dodoma na
inarajia kwenda Singida ili kuweza kuwaelimisha wazalishaji na
wauzaji namna ya kuyatunza mafuta ili
yawe na ubora.
“ Tumeenda kongwa kibaigwa hapa tutaenda manyoni
singida tutaendelea kusambaza elimu hii japo Kuna changamoto ambazo tunazipata
lakini nasi tunaziwekea mikakati
kiukweli kama mafuta yasipofungashwa vizuri kwa kupigwa na mwanga wa jua
mafuta yanaweza kuharibika”
Amesema
katika mafunzo hayo wanasisitiza katika uhifadhi ndio maana wanawatembelea wauzaji wa barabarani waweke vibanda kukinga
mafuta kwani jua linapopiga mafuta
yanaharibika.
Naye
Daudi Makala, mzalishaji mdogo wa mafuta
ya alizeti amesema amejifunza namna ya
kuzingatia ubora wa mafuta kwani kwa
kufanya hivyo atampa uhakika mtumiaji .
Pia tuhakikishe mbegu imekomaa na usafi pamoja na utayalishaji wa mafuta haya kiukweli tumejifunza mambo mengi tukizingatia nafikiri walaji watafurahia ,sisi wasindikaji wa mafuta inabidi sasa mara kwa mara tuwe na semina ili tuweze kukumbushana
Daudi Makala
Kwa upande wake Yunice Maneno muuzaji kutoka soko la saba saba amesema kutokana na
semina amejifunza mambo mengi kutoka kwa
mkulima hadi kufikia mafuta yenyewe .
“ Wakati mwingine unaweza kununua mafuta
machungu kumbe kutokana na mkulima kukimbilia soko anaweza akakamua
mafuta ambayo mbegu haijakauka kwahyo mi
niombe tu semina hizi tuzipate mara kwa mara na niwaombe wananchi watumie
mafuta haya ya alizeti kwani ni mazuri kwa afya”.Amesema Yunice.
0 Comments