📌NA HAMIDA RAMADHANI
TAASISI za umma nchini zimetakiwa kuzingatia
kikamilifu Sheria ya Serikali Mtandao ya mwaka 2019 na Kanuni zake za mwaka
2020 katika kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao mahala pa kazi.
Hayo, yameelezwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa
Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, ACP Ibrahim Mahumi kwa niaba ya Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.
Laurean Ndumbaro wakati akifungua mafunzo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo vya
TEHAMA Serikalini yaliyohusu kujenga uelewa katika utekelezaji wa Sheria ya Serikali
Mtandao na Kanuni zake.
ACP Mahumi ameeleza kuwa, Serikali kupitia Tangazo
Na. 964 la tarehe 6/12/2019, ilitangaza kuwa tarehe 15 Disemba 2019 ni siku ya
kuanza kutumika rasmi kwa Sheria hii ya Serikali Mtandao na Kanuni zake
zilizopitishwa mwanzoni mwa mwaka 2020 ambazo nazo zimeanza kutumika katika
kutekeleza sheria hii.
“Tambueni
kuwa Sheria hii inaweka msingi wa kisheria wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya
TEHAMA ya mwaka 2016 na kuanzisha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) yenye
jukumu la kusimamia, kuratibu na kuendeleza utekelezaji wa Serikali Mtandao,
pamoja na kusimamia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya
Serikali Mtandao katika taasisi za umma,” ACP Mahumi amesisitiza.
Aidha, ACP Mahumi amesema kuwa mafunzo haya ni moja
ya jitihada za kuongeza uelewa wa mambo ya kuzingatia wakati wa kutumia TEHAMA
katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika taasisi za umma na utoaji wa
huduma kwa umma, kwa lengo la kuongeza tija na kutoa huduma bora zinazopatikana
kwa urahisi.
Nazipongeza taasisi za umma ambazo zimefanikiwa kuboresha utendaji kazi na kutoa huduma zao kwa umma kwa kutumia TEHAMA, ingawa tunaelewa kumekuwa na changamoto katika eneo hili, kama vile uwepo wa mifumo isiyoongea na urudufu. Hivyo, sheria hii itasaidia kutatua baadhi ya changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na kuiwezesha Mamlaka ya Serikali Mtandao kutoa viwango na Uadilifu , Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
Amesema pia miongozo ya kitaalamu vya serikali
mtandao kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa jitihada mbalimbali za serikali
mtandao katika taasisi za umma.
ACP Mahumi ameendelea kusisitiza umuhimu wa kuzingatia vipengele vyote vinavyohusu usalama wa mifumo na miundombinu ya TEHAMA kama vilivyoainishwa katika Sheria ya Serikali Mtandao na Kanuni zake. Uzingatiaji huo utahakikisha usalama wa taarifa za Serikali zilizomo katika mifumo na miundombinu ya TEHAMA inayotumika katika taasisi za umma.
“Ingawa mafunzo haya yametolewa kwa Wakuu wa
Idara/Vitengo vya TEHAMA, ACP Mahumi amewaasa wakuu hao kuhakikisha na wao
wanakuwa walimu kwa kusaidia kuwaelewesha watumishi wenzao katika taasisi zao
kuifahamu na kuizingatia sheria hii na kanuni zake wakati wa utekelezaji wa
jitihada za Serikali Mtandao,’’amesema.
0 Comments