VYAMA VYA SIASA VYATAKIWA KUWAPA NAFASI YA JUU WANAWAKE KWENYE SIASA



 ðŸ“ŒNA HAMIDA RAMADHANI

IMEBAINIKA kwamba Vyama vingi vya Siasa vinawatumia wanawake katika shughuli za uhamasishaji katika kuongea idadi ya  wanachama na kueneza  Sera za chama ikiwemo wakati wa kampeni katika kuwavuta wapiga kura   lakini haimuoni mwanamke kama mdau  kwa ajili ya nafasi ya uongozi.

 Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Kamati  za Amani na  Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam   Alhad  Mussa Salum kwenye warsha  iliyoandaliwa na Chama Cha waandishi wa Habari wanawake (TAMWA) inayolenga nafasi ya mwanamke kuelekea uchaguzi mkuu october 2020,katika mustakabali  wa haki  heshima  aman na utulivu katika kuchagua viongozi bora.

 Amesema vikwazo hivyo ni pamoja na nguvu ndogo ya mwanamke kiuchumi , rushwa,lugha zalilishi, mila potofu  na wakati mwingine inasababisha baadhi ya wanawake kushindwa kujiamini  katika kukabiliana na vitendo  vya ukatili wa kijinsia.

Pamoja na changamoto hizo sote tumekuwa  tukishuhudia namna ambavyo wanawake kadhaa ambao walipata fursa ya kuongoza waliweza kuongoza kwa ustad na weledi mkubwa wakati mwingine kuliko hata wanaume 

Alhad Salumu.

Ameongeza kuwa  hayo yote na mengine  mengi wanawake ni watu wenye nguvu na uwezo katika uongozi hivyo wapewe nafasi kwa kuwachagua kwaajili ya maendeleo ya taifa tukiamini wazi wataendeleza vita ya rushwa,ufisadi,dawa za kulevya, na mengine mengi   kwa ustawi wa taifa ikiwemo  kusimamia haki za  wanyonge. 

Amesema kamati ya amani inaamini kwamba wanawake akichaguliwa katika nafasi ya uongozi  atakuwa na fursa ya kutunga sera na kushiriki katika vyombo vya maamuzi ambapo maendeleo na mapinduzi makubwa katika taifa la Tanzania yatatokea. 

"Ikumbukwe kwamba wanawake ni zaidi ya nusu ya idadi ya wanawake duniani hivyo ili kutokomeza umasikini ni lazima wanawake wapewe nafasi na kushirikishwa kikamilifu katika uongozi sasa nafasi imefika mwanamke achaguliwe  na kuwekwa mbele kwani tunaamini atafanya mambo mengi na kwa ufanisi zaidi" amesema Alhad Salumu

Pia ametoa wito wao  kama viongozi wa dini na viongozi wa amani  ni kuona vyama vya siasa na watanzania wote Kwa ujumla wanahitaji kuchagua viongozi walio bora ikiwemo wanawake  kwaajili ya maslahi mapana ya taifa kwa vizazi vya sasa na vitakavyokuja. 

Kwa upande wake mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake (TAMWA)Rose Ruben  amesema ushiriki wa wanawake katika siasa  na katika  ngazi ya maamuzi ni eneo lililo na changamoto lukuki  na hivyo inahitaji kuhimizwa na uongozi wa ngazi za juu, asasi za kiraia, wanawake wenyewe na viongozi wa dini. 

Takwimu zinaonesha kwamba ni asilimia 37 tu ya wanawake ndio waliopo katika ngazi za maaumuzi bunge lilopita, hata hivyo bado tunaona kuna mapengo katika ushiriki wao ambayo hayana budi kuzibwa

Rose Ruben

 




Ameongeza kusema kuwa " Mapengo hayo ni pamoja na lugha zalilishi wakati wa uchaguzi zinazowakatisha tamaa wanawake kuwania nafasi za uongozi, uteuzi usiozingatia jinsia katika ngazi ya siasa hofu na kutojiamini kwa wanawake  wenye nia ya kugombea na ilani za vyama visivyozingatia jinsia "amesema Rose

Aidha amesema mapengo mengine yaliyobainika ni pamoja na rushwa ya ngono yanatotajwa kutumika katika uchaguzi, rushwa ya kifedha, uchumi duni kwa wanawake  wanaotaka kugombea na hivyo kupelekea kushindwa kufanya kampeni, mila na desturi kandamizi  zinazowazuia wanawake kushiriki katika kampeni.

Amesema TAMWA inawasihi viongozi wa dini kuendelea kuhimiza wanawake kushiriki katika  siasa na ngazi za maamuzi  kwani wanaaminika Katika jamii. 

"Viongozi wa dini mna nafasi kubwa katika jamii kuondoa mila na mitazamo potofu inayochochea ushiriki duni wa mwanamke katika siasa na katika ngazi ya maamuzi, na pia wanatakiwa wahubiri amani na mshikamano katika kipindi cha uchaguzi na amani hiyo itapatikana iwapo makundi yote maalumu wakiwemo watu wenye ulemavu na mshikamano watashiriki kikamilifu katika uchaguzi "amesema Rose 

MKUU WA WILAYA YA DODOMA

Kwa upande wake Mkuu  wa Wilaya ya Dodoma Mjini  Josephat  Maganga akimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dodoma   Dk Binilith Mahenge amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuhakikisha wanadumisha aman utulivu na umoja hasa katika kipindi hiki cha kuelekea  uchaguzi mkuu 2020. 

Amesema kumekuwepo  na muamko mkubwa kwa wanawake kuwania nafasi mbali mbali za uongozi Toka 2015 lakini kwa mwaka 2020 idadi ya wanawake imeongezeka zaidi tena wenye sifa. 

Wanawake sasa wamekua wajasiri na wengi wameonesha wana uwezo wa kufanya kazi kubwa  tena iliyotukuka

Josephat Maganga .

 

 

Post a Comment

0 Comments