WATANZANIA WASHAURIWA KUTOWACHAGUA WANAOSAKA USHINDI KWA 'SANGOMA'

 


📌NA HAMIDA RAMADHANI


WATANZANIA wameshauriwa kutowachagua baadhi ya wagombea wanaowania  nafasi mbalimbali za uongozi ambao wameonekana wakipita kwa waganga wa kienyeji (sangoma) ili washinde kwa kishindo.


Ushauri  huo umetolewa na Askofu wa Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania, Kanda ya Kati Julias Bundala alipokuwa akiendesha ibada ya kuwaweka wakfu viongozi mbalimbalimbali wa kanisa hilo iliyofanyika Makole Jijini Dodoma.


Katika ibada hiyo ambayo iliambatana na wiki ya akina mama wa kanisa hilo kutoka kanada ya kati pamoja na kufanya uchaguzi wa viongozi wa akina mama, Askofu Bundala amesema kuwa katika uchaguzi kuna baadhi ya watu ambao wanatafuta madaraka kwa nguvu za giza.

Tumekuwa kutishuhudia katika kipindi cha uchaguziyanatokea mambo mbalimbali ambayo ni machukizo mbele za Mungu, wapo watu ambao wanatafuta uongozi kwa kusaka ngozi za albino, wengine watoto wadogo na wakati mwingine kufanya kafara ambazo wanaamini kuwa watapata uongozi.

Askofu Bundala.

“Kwa kipindi hiki amabcho kampeini zinaendelea na watu wanaendelea kuelezea sera zao hakikisha mnamchagua mtu ambaye anaweza kuongoza watu kwa manufaa ya watu wote lakini siyo yule ambaye anaviashiria vya kwenda kwa waganga wa kienyeji kwani mtuambaye anaweza kwenda madarakani kwa nguvu za giza hawezi kuwa kiongozi mzuri wa kuwatumikia watu” amesema Askofu Bundala.

Katika hatua nyingine Askofu Bundala amewataka watanzania kuwachagua viongozi ambao wanaonesha nia ya kuwatetea watanzania wote kwa misingi ya haki badala ya kuwakandamiza na kuwasababishia umasikini.

“Tanzania tunazo rasilimali nyingi na za kutosha, kwa sasa kuna wagombea wengi ambao wananadi sera zao lakini nawaomba watanzania wasikilizeni wagombea wote na chagueni watu ambao kimsingi wanaonesha nia ya kusimamia haki na maendeleo ya watu ili kuweza kuwafanya watanzania wote wawe wanufaika na rasilimali zilizopo.

“Tusiwe washabiki wa sera na kufanya maamuzi ambayo baadaye yanaweza kuwa majuto lazima tumchague kiongozi mwenye uchungu na maendeleo ya watu kwa faida ya watu wote na siyo watu wachache tu, na ili kuweza kumchagua mtu ambaye anaweza kusimamia haki ni wajibu wa wale wote wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi na kwa wakati kupiga kura kwa lengo la kumchagua kiongozi bora na siyo bora kiongozi” amesema Askofu Bundala.

Akizungumzia haki amevitaka vyombo vyote vya usalama pamoja na tume ya uchaguzi kuhakikisha inatenda haki kwa vyama vyote bila kupendelea chama chochote cha siasa ili kuepusha malalamiko ambayo yanaweza kujitokeza.

Amesema ili kuiweka nchi katika usalama ni lazima haki itendeke kwa vyama vyote na yule ambaye ataonekana kuwa ameshinda kwa kupigiwa kura atangazwe huyo na vyombo vya dola view vyombo vya kulinda usalama wa raia na mali zake sambamba na kutenda haki kwa vyama vyote kwa kutimiza sheria, taratibu na nanuni zao za kazi.

 

Post a Comment

0 Comments