DIWANI KILIMANI AFUNGA 'KAZI'



 ðŸ“ŒNA BARNABAS KISENGI 

MGOMBEA wa Udiwani wa Kata ya Kilimani jijini Dodoma Neema Mwaluko amewaomba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wa kata hhiyo kuhakikisha siku ya kupiga kura wanachagua wagombea wote kutoka chama hicho ili waendelee na juhudi za kuwaletea maendeleo

Akihitimisha kampeni zake katika kata hiyo Mwaluko amesema hiyo ndiyo Kata pekee ambayo wanaishi viongozi wengi wa serikali, hivyo inatakiwa iongozwe na diwani wa CCM ambaye atatatua kero mbalimbali zilizobaki katika Kata hiyo ikiwemo miundombinu ya barabara za mitaa

Neema amesema katika mitaa nyingine ya Kilimani tayari wameshatandaza barabara za ndani za lami  hiyo watakapo mpatia miaka mitano tena atahakikisha miundombinu ya barabara ya zilizobakia zinakamilika. 

 Pia mgombea huyo anayetetea kiti chake amesema atahakikisha anaanzisha ujenzi wa shule ya msingi wa Kata, zahanati,soko na kituo cha police katika kata hiyo ambayo kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto ya shule ya msingi ya Kata ambapo watoto wa Kata ya kilimani wanasomea shule ya msingi ya kata ya jirani.

Ameongeza kuwa  kwa sasa katika zoezi la upimaji lililofanyika katika mtaa wa Chinyoyo tayari wameshatenga eneo la kujenga shule ya msingi na sekondari na huduma nyingine za kijamii kwa kushirikiana na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa huo Faustina Bendera ambaye alimtengea eneo hilo la miundombinu ya ujenzi wa taasisi hizo. 

Akifunga kampeni hizo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilimani Mzee Kiwaya amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatano 28-10-2020 na kuhakikisha  wanachagua kwa mtindi wa mafiga ili  iwe kata ya mfano kwa maendeleo kati ya 41 za Jiji la Dodoma  

Post a Comment

0 Comments