ELIMU USAFI WA MAZINGIRA KINGA MAGONJWA YA MLIPUKO




 ðŸ“ŒNA PENDO MANGALA

 

BAADHI ya Wakazi Jiji la Dodoma wameeleza kuwa  elimu dhidi ya usafi imewasaidia kuondokana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu tofauti na ilivyokuwa hapo awali huku wakiiomba Serikali kuendeleza elimu hiyo.

Hayo wameyaeleza  Jijini Dodoma wakati walipokuwa wakizungumza na  kituo hiki ambapo wamesema kutokana na wao kupewa elimu na wataalam wa afya imekuwa mkombozi kwao.

"Kiukweli  Sasa hivi tumekuwa na muamko dhidi ya usafi tofauti na hapo awali,kwani miaka ya nyuma tulikuwa tunaona usafi sio kipaumbele lakini sasa hivi tunajitahidi kufanya usafi katika mazingira yetu na pia tunazingatia kanuni zote za usafi ikiwa ni pamoja na kutumia vyoo bora.",amesema

Naye Mwenyeviti wa Mtaa wa Karume Kata ya Mnadani,Kyata Matwiga amesema wamekuwa na utaratibu wakuwahimiza wananchi kufanya usafi wa mazingira yao yanayowazunguka kila jumamosi na kila mwisho wa mwezi wakazi wote hujitokeza kufanya usafi mtaa wote jambo ambalo limezaa matunda.

“Tangu tuanze kuhimiza usafi na kusimamia hakuna takataka zinazozagaa ovyo pia magonjwa ya mlipuko hakuna,suala  ambalo limesaidia kujilinda na magonjwa ya mlipuko kwani tumejiwekea taratibu za kutoza faini ya shilingi elfu 50 kwa wananchi ambao hawafuati taratibu za usafi”,alisema.

Amesema wamekuwa wakishirikiana na uongozi wa Jiji la Dodoma katika suala la kusimamia usafi ikiwemo suala la vyoo bora ambapo mwamko umekuwa mzuri.

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa huduma za kiuguzi katika Hospitali ya rufaa Mkoani Dodoma Dkt Stanley Mahundo amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko kwa  kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira kwa kuhakikisha mazingira yanayowazunguka yanakuwa safi muda wote.

 Bw. Mahundo amesema kuwa kila Mtanzania anajukumu la kujilinda na kujikinga katika maeneo anayoishi ili kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko kwa kuhakikisha wanafanya  usafi wa mazingira yanayowazunguka.

Magonjwa ya milipuko ni magonjwa ambayo hayawi kwa muda wote, yanasababishwa na vitu maalumu na ndiyo sababu yakawa magonjwa ya milipuko mfano wa magonjwa hayo ya milipuko  ni kipindupindu,uti wa mgongo,homa ya matumbo na hivi karibuni kulikuwa na corona

Amefafanua  kuwa vyanzo vyake vinatofautiana , ugonjwa wa kipindupindu vyanzo vyake vinatokana na vijidudu vinavyozagaa katika mazingira machafu na huenezwa na nzi ambapo akivisafirisha na kuviweka katika chakula na vikiliwa ndipo vinasababisha kipindupindu.

Ameeleza kuwa ili jamii ijikinge ni lazima mazingira yawe safi kwani kipindupindu kinasababishwa na mazingira machafu,hivyo ni muhimu kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na hata  chakula kinatakiwa kuwa safi na salama kabla ya kutumiwa.

Ni muhimu kuhakikisha tunajizuia na magonjwa haya kwa jamii yetu inatakiwa mazingira yawe safi kwa mfano kipindpind kinaambikizwa na mazingira mchafu hivyo ili kujikinga nilazima kuwe na mazingira masafi na uishi katika usafi ili kuweza kujikinga na magonjwa ya milipuko

Amesisitiza kuwa magonjwa mengi ya milipuko yanasababishwa na uchafu na kueleza kuwa kwa nilazima kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kwani kipindi cha nyuma hasa maeneo ya vijijini hakukuwa na uelewa hasa katika maswala ya usafi.

“Katika miaka ya nyuma jamii haikuwa na uelewa juu ya magonjwa ya milipuko naishukuru sana Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa elimu katika jamii hasa vijijini na kuhamasisha usafi wa mazingira,kipindi cha nyuma tulikuwa hatuna utaratibu wa kusafisha mazingira hasa vijijini wengi hawakuwa na vyoo na hata utaratibu wa kutumia vyoo hawakuwa nao lakini saizi ni tofauti sana na miaka ya nyuma,’’alisema Dkt Mahundo.

Wakati huo huo ameeleza juu ya ungonjwa wa Corona ambapo amesema kuwa juhudi za serikali kuhamasisha swala la unawaji wa mikono na matumizi ya vitakasa mikono imesaidia sana kujilinda na corona.

Kama nilivyosema awali  magonjwa mengi ya milipuko yanasababishwa na uchavu ndio sababu ya kwenye Corona tulihimiza juu ya swala la unawaji mikono kila muda baada na kabla ya kula hii yote ni kuwa magonjwa haya yanasababishwa na uchafu

Ameipongeza Serikali kwa kuhakikisha watanzania wanavuka salama katika janga la Corona ambapo nchi zote tulikuwa katika janga hilo na alisema kuwa kwa sasa Tanzania hakuna Corona ila ni muhumu kuendelea kuchukuwa tahadhari kwa kunawa mikono na kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima

Dk. Mahundo amesema mikakati yao ni kuhakikisha wanendelea kutoa elimu kwa jamii dhidi ya kuzingatia na kuendeleza usafi ili kuondokana na magonjwa hayo ya mlipuko.

Naye Mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka Wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto,Dk Leonard Subi amesema kuwepo kwa kampeni ya Usichukulie Poa nyumba ni choo imesaidia kupunguza kaya zisizokuwa na vyoo ambapo  matumizi ya vyoo bora yameongezeka kutoka asilimia 6.1 mwaka 2015/2016  hadi asilimia 2 mwaka 2019/2020.

Vile vile vyoo bora vimeongezeka kutoka asilimia 40 hadi asilimia 63.7 ambapo kaya zenye vifaa maalumu vya kunawia mikono zimeongezeka kutoka asilimia 12.4 hadi asilimia 37.6.

Katika hatua nyingine amesema serikali imepeleka shilingi bilioni 2.6 katika Halmashauri nchini kwenda kuimarisha huduma za upatikanaji wa maji safi lakini pia upatikanaji wa vyoo bora katika vituo vya kutolea huduma ya afya.

Amesema kampeni hizo zikiendelezwa zitasaidia kuwakinga watu dhidi ya magonjwa yanayoepukika.

 

Post a Comment

0 Comments