JAMII YASHAURILIWA KUTUMIA TAKWIMU KWA MAENDELEO YA NCHI

 


📌NA HAMIDA RAMADHANI

MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dkt Albina Chuwa amesema Takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Mali ya umma nasio ya Serikali pekee Kama jamii inavyodhani.

Ameyasema hayo Leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya takwimu Duniani ambapo amesema Tanzania leo inaungana na nchi zingine Duniani kuadhimisha siku ya Takwimu  huazimishwa kila baada ya miaka mitano.

Dk Albina amesema kutokana na hali hiyo kila mtu anapaswa kutumia takwimu kwaajili ya Maendeleo na kuachana na dhana iliyopo ya kwamba takwimu ni mali ya Serikali.

 Aidha amesema baraza kuu la umoja wa mataifa mnamo tarehe 3 june lilipitisha adhimio namba 69/282 ambalo liliamua siku ya tarehe 20 Oktoba 2015 kuwa maadhimisho ya pili ya siku ya takwimu ulimwenguni na kuamua tarehe 20 Oktoba ya kila baada ya miaka mitano kuadhimisha siku hiyo.

Amesema katika salamu zake kwa baraza kuu la umoja wa mataifa September 2020 katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres alizikumbusha nchi wanachama za umoja huo kuendelea kulitilia mkazo suala la Takwimu na maendeleo yake.

Akimnukuu katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres"Katika kuyafanya maadhimisho haya ya siku ya takwimu Duniani kuwa ya mafanikio naziomba Serikali zote Duniani ambazo ndizo wazalishaji,watumiaji,na wanufaika wakubwa wa takwimu rasmi kuweka jitihada zao kuunga mkono maadhimisho hayo "

Katika salamu zake hizo Guterres ameeleza kuwa takwimu za uhakika zinazotumika na zinazozalishwa kwa wakati ni muhimu katika kuielewa dunia inavyoishi hivi sasa na kuongeza kusema kuwa" Takwimu ni muhimu katika kufanya maamuzi ya kisera katika kila sekta na kwa jamii zote bila kujali tamaduni na historia zao au ngazi ya Maendeleo iliyofikiwa"alisema Guterres

AKIZUNGUMZIA JANGA LA CORONA.

Amebainisha kuwa janga la Corona limeongeza umuhimu wa data na takwimu na limeionesha dunia ni kwa namna gani taarifa za kijiografia zinavyoweza kusaidia kufatilia kasi ya mwenendo wa mabadiliko ya dunia.

Aidha Mkurugenzi wa idara ya takwimu ya umoja wa mataifa Stefan Schweinfes katika barua yake kwa jumuia ya takwimu Duniani amesema kuwa wakati nchi zetu zikizidi kuifanya mifumo ya takwimu kuhimili mabadiliko ya mahitaji kutokana na janga la Corona maadhimisho ya siku ya taifa ya takwimu yamekua na umuhimu zaidi kuliko yaliyopita.

Akimnukuu Schweinfes

kadri mifumo yetu ya takwimu inavyozidi kubadilika viwango vya Takwimu vyetu,uhuru wa mifumo wa taifa wa takwimu misingi ya takwimu rasmi inachangia na kuziongezea uaminifu data na takwimu zinazo zalishwa na mifumo yetu ya taifa ya takwimu na kutumika katika kufanya maamuzi

Dk Chuwa amesema tangu kupitishwa kwa azimio hilo mwaka 2015  Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbali mbali za kuendeleza na kuimalisha mifumo rasmi.

Pia amesema imeendelea kuboresha uwezo wa takwimu katika wizara,idara na taasisi za serikali kupitia Mpango wa kwanza wa  kuboresha na kuimarisha takwimu nchini.

Dk Chuwa ametoa wito kwa Umma na wadau wote kutumia takwimu katika kupanga Mipango ya Maendeleo ya nchi.

Siku ya Takwimu duniani huadhimishwa kila baada ya miaka mitano ambapo kwa mwaka huu imebebwa na kauli mbiu isemayo kuiunganisha  dunia kwa takwimu  tunazoziamini.

 

Post a Comment

0 Comments