NANE MBARONI KWA KUMILIKI SILAHA NA NYARA ZA SERIKALI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI


 


📌NA HAMIDA RAMADHANI

JESHI la Polisi Mkoani Dodoma limekamata jumla yawatuhumiwa Nane kwa makosa ya kupatikana na silaha pamoja na nyara za serikali kinyume na sheria za nchi.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini hapa Kamanda wa Polisi Gilles Muroto amesema kwa kushirikiana na vikosi vya kupambana na ujangili msako umefanyika katika maeneo mbalimbali na kufanukiwa kuwakamata watuhumiwa hao Nane.

Octobar 11 Mwaka huu majira ya saa 21: 00 usiku Katika Kijiji cha Ikingwa ,Kata ya Kinyasi,Tarafa ya Pahi ,wilaya ya Kondoa na mkoa wa Dodoma alikamatwa Nzara  Simon (21) akiwa na meno ya Tembo mawili ambayo ni nyara za serikali kinyume na sheria

Kamanda Muroto.

Na kuongeza kusema "Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani lakini msako mkali unaendelea dhidi ya watuhumiwa wengine,"amesema.

Aidha ameongeza kusema kuwa katika tukio la pili Kijiji cha Chaludewa ,wilaya ya Mpwapwa na mkoa wa Dodoma walikamatwa watuhumiwa watatuwakiwa na meno ya Tembo vipande viwili ambavyo ni nyara za serikali, kinyume na sheria.

Hata hivyo aliwataja  watuhumiwa waliokamatwa katika tukio Hilo nipamoja na Nchemba Masonga(75) mkazi wa Chaludewa Mpwapwa,SanyiwaNkubha (38) mkazi wa Kijiji cha Chibolu Mpwapwa na Daudi Nhimko(48) mkazi wa Kijiji cha Minjenja  Gairo upeleoezi unaendelea na upeleoezi ukikamilika watafikishwa mahakamani," amesema Kamanda Muroto.

Katika tukio la Tatu Kijiji na Kata ya Sejeli Tarafa ya Kongwa wilaya ya Kongwa mkoa wa Dodoma walikamatwa watatu wakiwa na silaha ya kivita Aina ya  AK 47 yenye namaba  UR2716 ikiwa na risasi zake 27 kwenye Magazine ambayo wakekuwa wakiitumia katika uhalifu wa kijangili.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Mngoya Juma(40)mkuluma,Amrini Mohamed (34)mkuluma Furaha Masaka(20)mkulima na wote ni wakazi wa Banyibanyi wilayani Kongwa.

Katika tukio la mwisho Mtaa wa Kisasa Medelii ,Kata ya Dodoma makulu, katika Jiji la Dodoma amekamatwa Daniel Masawe Madevu,(40)fundi ujenzi na mkazi wa Kisasa Medelii aliyekuwa akitafutwa kwa kosa la kumjeruhi kwa risasi Binti,sababu ikiwa ni ugomvi wa kimapenzi.

" Majeruhi amelazwa  ICU katika hospital ya rufaa Dodoma na anaendelea na matibabu,"amesema Kamanda Muroto.

Hata hivyo Kamanda amesema Mtuhumiwa alikamatwa akiwa na silaha Bastola Aina ya Browning Calb 7.65 Maker No A748082,Car No .95632 ikiwa na risasi Saba kinyume cha sheria na kuitumia katika uhalifu na kuhatarisha maisha ya watuhumiwa wengine.

Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini Silaha hiyo ameipataje na atafikishwa mahakamani mara upelelezi ukikamilika

 Kamanda Muroto.

Na kuongeza kusema kuwa"Hakuna mhalifu atakayebaki Salama , uhalifu haulipi na Kila mtu azingatie utii wa sheria kwa kufanya kazi halili," Amesema Kamanda Muroto.


Post a Comment

0 Comments