NDEJEMBI AFUNGA KAMPENI,AWAOMBA WANANCHI USHINDI WA KISHINDO

 


📌NA BARNABAS KISENGI

 

MGOMBEA  Ubunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma Deogratus Ndejembi amehitimisha kampeni zake katika jimbo hilo leo katika kata ya Haneti ambako pia Rais John Magufuli alisimama eneo hilo kuwasalimia wananchi akitokea mkoani Manyara.

Katika mkutano huo wa kufunga kampeni,Ndejembi amewaomba wananchi wa Chamwino kumchagua Mgombea wa CCM John Magufuli kwenye kiti cha Urais kwa kura nyingi za kishindo na kumchagua yeye awe mbunge wa Jimbo hilo na madiwani wote wanaotokana na CCM ili kutengeneza utatu wa kupeleka mabadiliko makubwa katika Jimbo la hilo.

Mkinichagua kuwa mbunge wenu nitawafanyia mambo makubwa hapa Jimboni ikiwa ni kuhakikisha kero zote za miundombinu, elimu, afya na mikopo inayotolewa na halmashauri ninaisimamia na kuitekeleza kwa kasi kubwa hapa jimboni

Ndejembi 

Awali akiwasalimu wananchi wa kata hiyo ya Haneti mgombea nafasi ya Urais kupitia CCM rais John Pombe Magufuli amesema ana mapenzi makubwa na mkoa wa Dodoma hivyo sababu iliyomfanya kuanzia kampeni mkoani hapa na kumalizia hapa pia.

Dodoma ninaipenda Sana na ndio maana mliponichagua tu 2015 nikahakikisha adhima ya hayati baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere ya Dodoma kuwa makao makuu nimeitekeleza kwa vitendo na serikali imehamia hapa na mimi na viongozi wengangu sasa wote tuko Dodoma makao makuu ya chama na serikali.

Magufuli

Mapokezi ya Mgombea Urais kupitia CCM  yameanzia wilayani Kondoa kupitaa Chemba na  kuhudhuriwa na viongozi wa chama mkoa na wilaya zote za Dodoma  ambapo rais amezungumza na wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi na kuwaomba kura za kishindo ili CCM iendelee kutawala na kuwaletea maendeleo kwa wananchi. 

 

Post a Comment

0 Comments