PROFESA MWAMFUPE AAHIDI MAKUBWA KATA YA MADUKANI

 


📌NA HAMIDA RAMADHANI


MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Madukani na aliyekuwa Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe ameahidi kutataua kero za umeme,ushuru na mapipa ya kuhifadhia uchafu kwa wafanyabiashara waliopo ndani ya kata hiyo alimaarufu (one way).

akiongea na wafanyabiashara hao katika kampeni ya mlango kwa mlango Profesa Mwamfupe amesema kata ya madukani ni kata ya wafanyabiasahara  hivyo lazima ahakikishe anafanya mambo makubwa ili kuhakikisha anaweka mazingira mazuri kwa wafanyabaiara wa kata  hiyo.

Mambo hayo  ni pamoja na mazingira mazuri ya wafanyabiashara kushushwa kwa kodi,wafanyabiashara wadogo wadogo alimaarufu (machinga) kutobughudhiwa na mtu yoyote

Mwamfupe

Aidha amesema katika suala zima la uboreshwaji wa biashara ni pamoja na kuweka taa katika eneo hilo ili wafanyabiashara wote wafanye kazi mpaka muda wa usiku au mpaka asubuhi ili wananchi wa kata hiyo na Dodoma kwa ujumla waweze kupata huduma hiyo.

Sasa hivi ukipita mida  ya saa  12  hadi saa 1  usiku maduka yote haya huyakuti yakiwa wazi yote  yanakuwa yamefungwa na niseme tu  hatukuja hapa eti tu ni kwasababu ya  kipindi cha uchaguzi  bali ni jukumu letu sisi kama viongozi kuhakikisha tunawaletea maendeleo wananchi

Profesa Mwamfupe.

Awali akitoa kero mbele ya mgombea udiwani huyo moja kati  ya wafanyabiashara hao Ferinanda  Sibo kero zinazowakabili  hapo ni pamoja na kukosa fursa za maendeleo kama vile kuomba mikopo kwa aajili ya kuendeleza biashara zao, pamoja na ushuru mkubwa.

"Juzi wamekuja hapa wametunyang'anya vichwa vya cherehani  kwasababu hatujalipa ushuru na gharama ni kubwa sana sasa wanapochukua vichwa vya cherehani na kuondoka navyo sisi hiyo pesa ya ushuru tutaitafutaje hali ya kuwa vitendea kazi wamevichukua"amesema  Ferinanda 

Kampeni ya mlango kwa mlango bado inaendelea ambapo leo imefanywa katika  barabara ya sita,barabara ya saba na barabara ya nane lengo likiwa ni  kutaka kujua kero ya mfanyabaiashara mmoja mmoja.

 

Post a Comment

0 Comments