Profesa Mwamfupe ahaidi kuibadili kata ya Madukani kuwa kama Kariakoo

 


📌NA HAMIDA RAMADHANI

MGOMBEA Udiwani kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM na aliyekuwa Meya wa Jiji la Dodoma Davis Mwamfupe ameomba ridhaa ya kuwa Diwani wa Kata ya Madukani huku akiahidi kuibadilisha Kata hiyo na kuwa Kama Kariakoo.

Akiongea jana katika mkutano wake  wa kampeni uliofanyika ndani ya kata hiyo barabara ya sita jijini hapa profesa Mwamfupe amewaomba wanamadukani wamchague ili aibadilishe Kata hiyo kwa kuyafanya mambo makubwa hasa kwenye suala zima la biashara zao.

" Ndugu wananchi endapo mtanipa ridhaa na kuwa Diwani wenu wa Kata hii ya Madukani nawahakikishia nitaibadilisha Kata hii na kuwa kama kariakoo kwanii inafahamika wazi uchumi wa Dodoma upo ndani ya Kata ya Madukani," amesema profesa Mwamfupe.

Aidha aliwapa pole wakazi wa Kata hiyo ya Madukani kwa kipindi cha miaka mitano kukosa muwakilishi wa uhakika na mwenye kuthubutu kuleta maendeleo ndani ya kata na wananchi kwa ujumla.

 "Wananchi ili kupata maendeleo chagueni viongozi wanaotoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt John Magufuli,Mbunge Antony Mavunde na Udiwani Mimi Profesa Davis Mwamfupe ndio tutakae leta maendeleo hayo," alisema Profesa Mwamfupe.

 Hata hivyo amesema yeye ni mzoefu katika masuala ya uongozi, utashi na anamoyo wa kuwatumikia wananchi ipasavyo na katika vipaumbele vyake vyote vinafanana na mahitaji na changamoto za wakazi wa Kata hiyo ya Madukani.

Amesema akipata nafasi hiyo ya uongozi atahakikisha anajielekeza katika kuwapatia wakazi wa Madukani huduma Bora za biashara na huduma Bora za kijamii ikiwemo kufunga taa kubwa katika barabara zote na kuwaongezea muda wa kufanya biashara wafanya biashara ambapo watafanya biashara muda wa masaa 24 .

Pia Amesema ataongeza vyoo Bora,mapipa ya kuifadhia taka na uzibuaji na upanuaji wa mitalo yanayopitisha majitaka .

Kwa Upande wa Vijana amesema Vijana  wengi wamekuwa wakitumika vibaya nà wengine kujiingiza katika mambo yaliyopelekea kughalimu maisha yao .

"Mimi nitakuwa mbele kuhakikisha changamoto zote zinazowakabili Vijana zinatatuliwa kwa kutoa mikopo isiyo na riba kwa wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu nafahamu makundi haya yote niliyoyasema wanavikundi vyaoa hivyo upatikanaji wa mikopo ya Jiji watapata," amesema profesa.

Kwa upande wake Mgombea  wa Ubunge kupitia CCM Dodoma mjini Antony Mavunde amewataka wananchi wa kata hiyo ya Madukani kumchagua Profesa Mwamfupe ili kuwaletea maendeleo ya muda mrefu waliokuwa wakiyawaza na kuyataka.

"Niseme tu Profesa Mwamfupe si mzee ni kijana  na uchapaji kazi wake tunaujua wakati akiwa Mstahiki Meya kwanza alienda nje kwenda kujiendeleza masuala mazima ya mazingira ,namna gani ya kufanya kazi bara bara na haya maendeleo madogo mnayoyaona katika kata hii ni  nguvu ya  Profesa Mwamfupe pindi alipikuwa Meya wa Jiji"alisema Mavunde

"Oktoba 28 siku ya kupiga kura msifanye makosa Rais mchagueni Dkt John Magufuli, Mbunge Antony Mavunde na Diwani Profesa Mwamfupe," amesema

 

Post a Comment

0 Comments