RC MAHENGE AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUHUBIRI AMANI

 


📌NA HAMIDA RAMADHANI

MKUU Wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amewataka Viongozi wa Dini kuhakikisha wanahubiri amani na utulivu katika kipindi hiki Cha kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 28 Mwaka huu

Amezungumza hayo leo jijini Hapa kwenye kikao cha kujadili masuala ya amani na utulivu katika mkoa wa Dodoma hasa katika kipindi hiki Cha kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 2020

Dkt Mahenge Amesema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi na zikiwa zimebaki siku chache itikadi za Udini,Ukabila na Ukanda zisiwepo ndani ya Mionyo ya watanzania Jambo kubwa la kilibabe siku ya Oktoba 28 ni kuimba na kuomba amani na utulivu ubaki pale pale.

Nchi yetu kwa muda mrefu imekuwa kisiwa Cha amani na tumekuwa wasuruhishi katika mataifa mingine hivyo amani yetu na utulivu tusiupoteze

Dkt Mahenge.

 Na kuongeza kusema,"Amani yetu na utulivu imetufanya na imetufanikusha kufikia uchumi wa kati hivyo amani ndio Msingi wa shughuli zote za kiuchumi," Amesema .

Kwa Upande wake Afisa Tawala mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa Prudensia Kwabila Amesema katika kipindi hiki Msajili anaviasa vyama wote vya siasa kuzingatia katiba na sheria za nchi 

Aidha amezitaja   sheria hizo nipamoja na Sheria  Gharama za uchaguzi pamoja, sheria ya vyama vya siasa pamoja na kanuni zake ili kudumisha Amani na utulivu mchini.

Naye Mwenyekiti wa Viongozi wa Dini mkoa wa Dodoma Shekhe Mustapha Rajabu Amesema katika kipindi hiki Cha uchaguzi kumeibuka sintofahamu nyingi na maneno ya ukakasi tena yakisemwa na Viongozi wetu wa dini.

Amesema Viongozi wa dini wamesahau majukumu yao ya kuhubili dini, utulivu na kumcha Mungu badalayake wamekuwa mameneja kampeni wa Mgombea na Chama fulani Cha siasa.

Sisi Viongozi wa Dini tuwe mstari wa kuwafundisha wahumini wetu matendo mema na  tuonyesha ni jinsi tunavyo muhitaji M/Mungu hasa katika kipindi hiki kwani sisi Viongozi wa Dini ni walezi wa jamii.

 Shekhe Mustapha.

Post a Comment

0 Comments