SHEKHE MKUU WA DODOMA AMKANA SHEKHE PONDA

 




📌NA HAMIDA RAMADHANI

SHEKHE Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mustapha Rajab amekanusha kauli iliyotolewa na shekhe Ponda issa Ponda kwamba waumini wote wa dini ya kiislam wamekubaliana kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao.

Hivi karibuni katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma wa mgombea urais kupitia chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),sheikh Ponda alitoa kauli aliyodai kwamba waislam wote wamekubaliana kumchagua Lissu kuwa Rais katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.

Akizungumza hijini hapa leo na waandishi wa habari baada ya Baraza la Masheikh wa mkoa na wilaya ya Dodoma,Sheikh Mustapha amesema kauli aliyoitoa Ponda siyo ya waislam wote bali ni kauli yake yeye mwenyewe na maslahi yake binafsi.

 

Amesema,hakuna mahali popote ambapo waislam wamekubaliana suala hilo na kama lingekuwepi basi msemaji Mkuu ambaye angepaswa kulitolea tamko ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber na siyo vinginevyo.

Sheikh Mustapha amewataka Masheikh na viongozi wote wa dini kwa ujumla kurejea makubaliano yao ya kuombea na kuwahimiza wananchi kuenzi amani na utulivu nchini hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

 

Tunalaani vikali tamko lililotolewa na Sheikh Ponda ,maneno yake yapuuzwe maana msemaji Mkuu wa Waislam ni Sheikh Mkuu wa Tanzania na si vinginevyo.

Ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha siku ya kupiga kura wanakwenda kupiga kura na kumchagua kiongozi wanayeona atawafaa katika kuwaletea maendeleo.

 

Post a Comment

0 Comments