TAKUKURU YAOKOA BILIONI MOJA NA KUIREJESHA SERIKALINI

 


📌NA DOTTO KWILASA

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU )mkoa wa Dodoma imeokoa zaidi ya shilingi za kitanzania Bilioni 1 na kuzirejesha serikalini na kwenye vyama vya Ushirika. 

Aidha TAKUKURU imesema katika fedha hizo sh.milion 323.681,100 ambazo zinajumuisha fedha walizolipwa wakandarasi kinyume na mikataba. 

Akizungumza na waandishi wa habari  Jijini  hapa,Mkuu wa TAKUKURU mkoani Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema fedha hizo zilikusanywa kutoka katika malipo ya watumishi wa umma,madeni,Saccos na za mikopo umiza.

Licha ya hayo ametoa ufafanuzi kuhusu fedha hizo kuwa kiasi cha sh.Milioni  81 zimereshwa na wakandarasi na watumishi wa TARURA waliolipwa bila kustahili. 

"Takukuru imefanikiwa pia kurejesha viwanja sita vyenye thamani ya sh milion 72 waliokuwa wamedhulumiwa haki yao, "anasema Kibwengo. 

Ameongeza kuwa , fedha zilizorejeshwa kuanzia Juni 2020 zimefikia sh 104,460,557 kati ya sh. 124,514,024 zinazopaswa kurejeshwa. 

Amesema kuna fedha pia ambazo zimerejesha sh milion 18 za mstaafu ambaye mwaka 2016 alizotoa kwa kampuni moja ili apewe trekta Kisha kampuni hiyo kushindwa kutimiza .

Kibwengo amefafanua zaidi ya kuwa sh. milioni 950,300,000 ziliokolewa na ushirikiano na Ofisi ya Mthamini Mkuu wa serikali baada ya kufanya uhakiki wa ndani na kwenye jedwali ya fidia kwa wananchi waliotwaliwa ardhi zao kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko wa nje jijini Dodoma. 

Katika kuhakikisha kwamba miradi ya maendeleo inafanyika kwa weledi na thamani halisi ya fedha inapatikana tumekagua miradi 19 yenye thamani ya zaidi ya sh bilion 6;

Aidha katika sekta ya za Maji, Ujenzi  afya na Elimu ambapo hatua mbalimbali zilikuwa zimechukuliwa ikiwemo kutolewa maelekezo ya marekebisho ya baadhi ya dosari"anasema 

Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma ameongeza kuwa wao wakiwa mabalozi wa kupambana na vitendo vya rushwa ,wanaendelea na uchunguzi wa shilingi milioni 245 baada ya viashiria vya jinai kuonekana katika miradi miwili ya maji wilayani Kongwa yenye thamani ya sh 1,538,417,421.

Katika hatua nyingine amezitaja sekta zinazoongoza kulalamikiwa na Wananchi kuwa ni  Ardhi  kwa asilimia 60,ikifuatiwa na vyama vya Siasa kwa asilimia12,huku Ujenzi ikiwa na asilimia tano, mikopo Umiza asilimia tano na polisi asilimia nne.  

Amesema pia wamepokea taarifa 482 za rushwa, na wamekamilisha uchunguzi wa majalada 16 na kufungua mashauri 15.

Tumefanya uchambuzi wa mifumo ya utendaji na utoaji huduma katika sekta ya kodi,afya na fedha za kuendesha warsha.

Kibwengo

Post a Comment

0 Comments