TEWA AMEWAOMBA WAGOMBEA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU

 


📌NA DOTTO KWILASA

KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mohammed Seleman Tewa amewaomba wagombea wa nafasi mbalimbali kufanya kampeni za kistaarabu kama zinazofanywa na Mgombea CCM,John Magufuli.

Amesema kufanya kampeni za kistaarabu kutasababisha amani kuendelea kuwepo kwenye jamii kwani licha ya maisha ya siasa bado Kuna maisha mengine ambayo yanategemea zaidi amani ,usikivu na ushirikiano.

Kauli hiyo ameitoa Jijini hapa wakati  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya  mwenendo wa kampeni nchini,ambapo Tewa alisema Mgombea wa nafasi ya urais, John Magufuli anafanya kampeni za kistaarabu hivyo na wagombea wa nafasi zingine za ubunge,udiwani pamoja na urais kwa vyama vingine  wanatakiwa kuiga mfano huo.

Kada huyo amesema Magufuli amekuwa kinara wa kueleza amefanya nini na akichaguliwa tena kwa mara nyingine atafanya nini tofauti na vyama vingine ambavyo vimekuwa vikishindwa kutoa sera zao na kujikuta wakitoa matusi.

Wajifunze kwa Magufuli (Mgombea wa CCM) kwanza anafanya siasa za kistaarabu,anawatambulisha wabunge na madiwani kasha anaelezea atafanya nini kwa kipindi kingine,huku akieleza kwa miaka iliyopita amefanya nini

Tewa.

Vilevile amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa ni chama cha kulalamika tu na kuchezewa faulo huku kikiwa hakielezi kitafanya nini.

Kada huyo pia amewaomba wagombea wote kutii maagizo yote yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi (NEC) ya wanapoitwa  watii maagizo kwani hao ndio wasimamizi wa uchaguzi.

Hata hivyo amesema licha ya kelele zote hizi zinazoendelea hakuna chama kinachoweza kushindana na CCM katika nafasi ya urais kwani mgombea wa CCM amefanya mambo makubwa kwa kuleta maendele ya watu pamoja na vitu.

Kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar amesema utakuwa mwepesi kutokana na mgombea wa urais,Hussein Mwinyi kukubalika kwa watu wote.

“Nawausia ndugu zangu wa Zanzibar wasikosee kule ni Mwinyi kwani uongozi anauweza na amefanya kazi ambazo kila mmoja anaziona,”amesema.

 

Post a Comment

0 Comments