WATU MILIONI 4.4 NDIO WANUFAIKA WA MFUKO WA BIMA YA AFYA

 


📌NA HAMIDA RAMADHANI

 

MKURUGENZI wa Sera na Mipango kutoka idara kuu ya Afya Edward Mbanga amesema kuwa Jumla ya Watu Milioni 4.4 ndio wanufaika wa mfuko wa Taifa wa bima ya  afya nchini NHIF.

Kauli hiyo ametolewa Jana jijini hapa alipokuwa akifungua kikao kazi kilichowakutanisha wahariri wa habari katika kujadili huduma za mfuko wa bima ya afya zinavyokwenda.

Amesema Tanzania ina jumla ya Watu Milioni 60 lakini wanufaika wetu au Watu waliojiunga na huduma za bima ya afya ni Milioni 4.4.

"Idadi hii kwetu bado ni ndogo kwani lengo letu ni kuhakikisha tunafanikiwa kwa kila mtanzania kutumia huduma ya bima ya afya na kuachana na tabia ya kwenda kutibiwa kwa kutoa hela zao mifukoni," alisema Mbanga.

 Na kuongeza kusema" Serikali ipo katika majadiliano ya kuona hawa asilimia 26 waliobaki na wasiokuwa na pesa ya kujiunga na mfuko ni namna gani itaweza kuwakomboa juu kupata huduma Bora ya afya ," amesema

Aidha amesema kwamba ,serikali ipo katika harakati za kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na bima ya afya mchini..

Naye Mkurugenzi Mkuu Wa NHIF Bernard Konga amesema kuwa  wakati mfuko unaanzishwa ulikuwa na Watu wachache kutokana na Watu kulalamikia huduma.

Hata hivyo amesema maboresho makubwa yamefanyika hasa katika  suala zima la upatikanaji wa dawa ambapo ndipo malalamiko yalikuwa kwa kiasi kikubwa.

Tumepanua wigo wa upatikanaji wa dawa hasa kwenye upande wake vifurushi na tumefanikiwa kupunguza malalamiko ya wateja wetu

Benard Konga..

 Mfuko huo wa Bima ya Afya, mpaka Sasa unamiaka 19 tangia ulipoanzishwa mwaka 2001 na mkutano huo Kati ya wahariri na watumishi wa Bima ya Afya ni mkutano wake 5.

 

Post a Comment

0 Comments