AFISA AFYA KONGWA AFIKISHWA MAHAKAMANI,KISA? RUSHWA

 


📌HAMIDA RAMADHANI  

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imemfikisha mahakamani Afisa Afya Mkuu Msaidizi wa  Wilaya ya Kongwa  Anania Madono (57) kwa kushawishi kupokea rushwa ya Sh.200,000.

Uchunguzi umeonyesha kuwa mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu  mshitakiwa alikamata na kushikilia madumu 63 yenye lita 309 za mafuta ya Alizeti  kwa madai ya kwamba hayakuwa na vifungashio na alimtaka mmiliki ampe fedha hizo ili amuachie.

Akitoa taarifa hiyo  Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo alisema mtuhumiwa huyo alipokea rushwa Novemba 8 mwaka huu eneo la Kibaigwa wilayani kongwa na kurejesha madumu hayo kwa mmiliki baada ya kupokea fedha hizo.

Kibwengo alisema pia Takukuru imemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Elibariki  Mngahani (29 ) ambaye ni Afisa Uhamiaji na kumfungulia mashitaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa ya 500,000 kinyume na kifungu cha 15(1)cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Uchunguzi wetu umeonesha kwamba  Oktoba 3 mwaka huu majira ya saa 5 usiku  katika eneo la Dodoma Hotel mshitakiwa alishawishi na kupokea rushwa hiyo kutoka kwa Saulabh Tanwar kama kishawishi ili isaidie kuachiwa kwa Gange  Thangadurai, raia wa India ,ambaye alikuwa ameshikiliwa na maafisa wenzake wa uhamiaji kwa kosa la kuwazuia kufanya kazi yao.Kibwengo

Ameongeza kuwa “Tumemfikisha Hamisi Athumani (27) fundi magari wa kampuni ya Yapi Merkezi na kumfungulia mashtaka sita ya kushawishi na kupoikea jumla Sh.380,000 kutoka kwa wananchi watatu kinyume na kifungu cha 15(1)cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa,”ameeleza .

Kibwengo amesema Mahakama ya wilaya ya Bahi imetoa uamuzi wa shauri la jinai namba 46/2019 na  kumhukumu Daudi Masigati ,Mjumbe wa balaza la Ardhi kata ya chikole  aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka mawiliya kushawishi na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)cha sehria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2017.

Amesema mahakama imemtaka mtuhumiwa kulipa faini ya Sh.500,000 au kwenda jera kwa miaka mitatu kwa kila shitaka .

Uamuzi huo ulitolewa baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na TAKUKURU kufuatilia uchunguzi ulionyesha kwamba mwaka jana alishawishi na kupokea Sh.200,000 ili amsaidie mtoa taarifa wetu kushinda shauri lake la mgogoro wa ardhi lililokuwa linaendelea kwenye Baraza
Kibwengo

 

Post a Comment

0 Comments