FAHAMU SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ILIVYOFANIKIWA KUTOKOMEZA UGONJWA WA MALARIA

 



📌HAMIDA RAMADHANI 

IMEELEZWA kuwa Ugonjwa wa Malaria katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar umepungua kwa kiwango kikubwa hadi kufikia asilimia 0.5 kwa wagonjwa .

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Dkt Abdullah Ally kutoka Wizara ya afya Mpango wa kutokomeza Malaria Zanzibar alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Kongamano la saba la wadau wa afya Tanzania (Health Summit) liliofanyika katika ukumbi wa St Gaspar Dodoma.

Kama inavyofahamika Tanzania imeingia katika uchumi wa kati hivyo suala la malaria ni suala nyeti hivyo hatunabudi kuhakikisha tunapambana nalo kwa nguvu zetu zote.

Dkt Abdullah Ally

Amesema kwa upande wa Zanzibar ugonjwa wa Malarial umepungua kea kiasi kikubwa, ambapo amesema mbinu kubwa ikiwa ni pamoja na kutumia mfumo mpya wa ndege isiyokuwa na rubani au Ndege Nyuki inayoweza kutambua mazalia ya mbu kona zote.

Amesema pamoja na kuhamasisha Watu watumie vyandarua ,tafiti mbalimbali kufanyika lakini Sasa wameongeza wigo na kuja najia nyingine mbadala ya ndege isiyokuwa na rubani.

"Njia hii ya ndege isiyokuwa na rubani au ndege nyuki imetusaidia Sana Zanzibar ugonjwa wa Malaria kupunguza hadi kufikia asilimia 0.5 ambapo naweza kusema kwamba katika Watu 100 ukiwapima mmoja ndiye atakayekutwa na ugonjwa kwakweli tumepiga hatua," alisema Dkt Abdullah Ally.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Ndege isiyokuwa na rubani kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar Yussufu Said Yussufu amesema ndege hiyo isiyokuwa na rubani sio ngeni nchini na imekuwa ikitumika zaidi katika uperesheni za kijeshi,kutengeneza ramani na katika kilimo Sisi tunatuma ndege hii kwa kuua mazalia ya mbu," amesema Mkufunzi huyo

Amesema ndege imeweza kurahisisha kazi na imekuwa ikitoa taarifa ni kiasi gani cha dawa inatakuwa kutumia katika eneo fulani.

Utakuta kuna maeneo mengine hatarishi na  magumu kufikia lakini ndege nyuki hii imeweza kusaidia na kufanikiwa kunyunyiza dawa maeneo hayo hatarishi na hata sehemu nyinge yakiwemo kwenye mabwawa na mashamba ya mpunga.

Yussufu Said Yussufu

Na kuongeza kusema kuwa "Haya ni Maendeleo makubwa ya kuhakikisha tunaendelea kuhakisha tunaboresha afya za watu kwa kutukomeza malaria Tanzania bara na Zanzibar kwa njia ya ndege nyuki.," Amesema Mkufunzi huyo Yussufu

 

Post a Comment

0 Comments