HOSPITALI ZA RUFAA ZATAKIWA KUJIONGEZA KUWA WABUNIFU

 


📌HAMIDA RAMADHANI

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mabula mchembe amezitaka Hospitali za Rufaa kote nchini kujiongeza kwa kuwa na  ubunifu mahususi wa kutengeneza vitu mbalimbali kama kipindi cha korona jambo ambalo litasaidia Taifa kutokupoteza pesa kwenda nje ya nchi.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati alipokuwa kwenye Maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa Hospitali ya Rufaa Dodona (General) .

Aidha Katibu huyo amesema kuwa kuna haja ya Hospitali zote kuwa na ubunifu mbalimbali wa kutengeneza vifaa ambavyo nchi imekuwa ikitumia pesa nyingi kwenda nje ya nchi kuvinunua jambo ambalo sio sahihi kwani wapo wataalamu wenye vipaji na ujuzi mkubwa.

"Niwasihi msibweteke amka anzeni kutumia vipaji vyenu kulisaidia Taifa letu nakumbuka wakati wa kupindi cha Ugonjwa wa Korona mlijitahidi kutengeneza vifaa mbalimbali ikiwemo barakoa,vitakasa mikono na makoti hali iliyosaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma kiurahisi"

"Nashauri ni vyema kila Hospitali kuwepo na kitengo hicho na kitatengeneza maji ya Drip kwani wagonjwa wengi wamekuwa wakihangaika pale wanapokuta yameisha kwa kufanya hivyo itatusaidia Serikali na Hospitali kuwa maendeleo makubwa "amesema Katibu mkuu Profesa Mchembe.

Katika hatua nyingine amewataka wafanyakazi kuwa na kasumba ya kufanya kazi kwa upendo,kusaidiana ,kuelekezana,kufundishana,kujifunza na kushirikiana kwa watu wote bila kujali vyeo walivyo navyo na kwa kufanya hivyo huduma itafika mbali .

"Na katika kufanikisha shughuli za ujenzi  niwashauri muwe mnawatumia watu wa magereza ambao watafanya kwa haraka na gharama nafuu na pesa zinazobaki zitasaidia kufanya kununua madawa"amesema

Nae Mganga mfawidhi wa Hospitali ya General Daktari Ernest  Ibenzi amesema tangu kuanzishwa kwa hispitali hiyo kupitia Serikali  na waasisi mbalimbali waliopitia ambao walifanya kazi kubwa ya kuboresha miundo mbinu.

Kuwa mbali na mafanikio makubwa yaliyopo katika utoaji huduma za afya bado kuna changamoto licha ya  Serikali ikuendelea  kuzitatua .

"Bado tuna upungufu wa watumishi, Majengo mbalimbali na ukosefu wa uzio imara,vifaa na  majengo ya mifupa tunaomba Serikali iweze kutusaidia ili tuweze kufanya kazi kwa viwango stahiki"amesema Daktari Ibenzi. 

Bertha Bahati ni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo amesema kuwa huduma inayotolewa inaridhisha kwani wanapata madawa kwa wakati,wanasikilizwa vizuri tofauti na kipindi cha nyuma ambapo manesi walikuwa wanawanyanyapaa na kutoa kauli mbaya kwa wagonjwa.

"Tunamshukuru sana Rais wetu John Magufuli amerudisha heshima kwenye Hospitali nyingi siku hizi unapofika hospitali tunapewa huduma zote na kwa haraka na hakuna tena ubaguzi kama zamani ambapo ungekaa kwenye foleni asubuhi mpaka jioni bila kusikilizwa na kunyanyapiliwa"amesema Bertha.

 

Post a Comment

0 Comments