MAGONJWA YA MLIPUKO:USAFI NI SULUHISHO PEKEE?

 


 ðŸ“ŒHAMIDA RAMADHANI

IMEELEZWA kuwa magonjwa ya mlipuko ni magonjwa yanayoenea kwa kasi na kwa muda mfupi na kuathiri kundi  la watu wengi katika jamii.

Toka dunia tuijue kuna magonjwa mengi ya mlipuko yakiwemo Tauni,Mafua ya hispania,ukimwi Mafua ya nguruwe,Kindupindu na Ebola .

CHANZO CHA MAGONJWA YA MLIPUKO.

Chanzo cha magonjwa ya mlipuko kinaweza kikawa kimoja au viwili lakini chanzo kikubwa ni uchafu,kutonawa mikono baada ya kutoka chooni kwa maji safi tiririka na sabuni ,kutokuweka mzingira katika hali ya usafi.

Lakini pia chanzo kingine ni kusambaa kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu mfano ugonjwa wa zika ambao unaambukizwa na mbu na ugonjwa wa kimeta unaoambukizwa kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.

Daktari bingwa kutoka kitengo cha magonjwa ya dharula katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, Dkt. Mathew Mushi amesema baada ya kupambana na magonjwa ya mlipuko huko nyuma kidogo na Dunia kufanikiwa kupata chanjo na tiba kwa sasa dunia inapambana na gonjwa la Corona (Covid 19).

Ugonjwa wa Corona ulianza mwezi wa 12 mwaka jana ambapo mpaka sasa ni mwaka na umeathiri sehemu kubwa ya ulimwengu.

Ugonjwa wa Corona unaenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kwa njia ya hewa au maji maji kutoka kwa mtu alieathirika kwenda kwa mtu mwingine.

Dkt Mushi amesema ili kumgundua mgonjwa alieambukizwa ugonjwa wa Corona inachukua siku 3 hadi 6  kwa mgonjwa kupatiwa na dalili za homa kali kikohozi,kuchoka mwili maumivu ya viungo, kukosa ladha ya chakula.

NAMNA YA KUJIKINGA.

Dkt Mushi ameishauri jamiii izingatie usafi na maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya ikiwemo kunawa mikono kwa maji safi yanayo tiririka na sabuni ,kutumia vyoo bora na Safi, kuvaa barakoa,na kama mtu ana dalili ya homa kali za mafua kaa nae mbali angalau mita moja.

Jamii itambue kwamba ugonjwa wa Corona hauna kinga wala chanjo  licha  ya shirika la afya duniani  WHO kufanya jitihada na  kutafuta  Kinga, chanjo na tiba ya ugonjwa huu.
Dkt Mushi .

Na kuongeza kusema "Katika  watu wapatao mia moja wenye maambukizi ya homa kali ya mapafu vifo vinaweza vikawa viwili hivyo siyo ugonjwa wa kutisha "amesema Dkt Mushi

Aidha amesema kuwa siyo magonjwa yote ya mlipuko hayana chanjo wala tiba lahasha bali kuna ugonjwa kama Polio, Tauni,Ukimwi Ebola yote yamepata chanjo hata ugonjwa wa Corona nao upo mbioni kupatiwa chanjo.

Magonjwa ya mlipuko ni magonjwa hatarishi hivyo jamii imeaswa kuzingatia ushauri unaotolewa na matabibu

Dkt Mushi

HALI YA CORONA KWA UPANDE WA TANZANIA

Mpaka sasa nchini Tanzania hakuna visa au taarifa yoyote ya uwepo wa mgonjwa yoyote aliebainika kuwa na kirusi cha ugonjwa wa Corona (Covid 19).

Dkt Mushi amesema kwa mujibu wa Takwimu kutoka wizara ya afya za mwezi wa nne mwaka huu 2020 zilizowasilishwa na aliyekuwa Waziri Wa Afaya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watatoa Ummy Mwalimu  zilisema kwamba wagonjwa wa mwisho kubainika na  Corona walikua ni watu 500.

NAMNA YA KUISHI KWA WAGONJWA WANAISHI NA MAKONGJWA SIO AMBUKIZA

Katika ugonjwa wa Corona Watu wanaoishi na magonjwa yasiyo ya kuambukiza  ikiwemo magonjwa ya kisukari,saratani  presha wapo hatarini kupatwa na gonjwa la homa kali ya mapafu kutokana na kinga zao za mwili kuwa dhaifu. 

Licha ya Tanzania  kutokuwepo kwa ugonjwa huo wa corona wataalam wa afya  walitoa ushauri na wanaendelea kushauri watu wote wenye magonjwa  yasiyo ambukiza wazingatie ushauri wa wataalam wa afya ili kujikinga na magonjwa nyemelezi.

Kutokana na kinga zao kuwa  ndogo  wagonjwa wote  wanashauriwa  kutulia nyumbani kuzingatia usafi  na kufanya mazoezi.
Dkt Mushi

Sambamba na hayo wagonjwa hao wanashauriwa kuzingatia mlo kamili kutoka kwenye makundi yote ya chakula ili kuendelea kuimarisha miili yao.

Wagonjwa wanashauriwa kutumia mafuta kidogo  ya kula na yanayotokana na mimea,ikiwemo alizeti,karanga ubuyu ufuta, pamoja na michikichi ili kuendelea kuimarisha miili yao.

Pia wanashauriwa kutumia dawa kama walivyoshauriwa na madaktari ili kuendelea kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

 

Post a Comment

0 Comments