📌RHODA
SIMBA
MRADI wa Tuimarishe afya wa
(HPSS) unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi chini ya shirika la
Maendeleo la SDC Swiss Agency For Development and Copperation
umejipanga kuboresha mfumo mzima wa afya nchini kwa kutekeleza
miradi mbali mbali kupitia serikali.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na
Meneja mradi Ally Abdallah wakati akizungumza na waandishi wa
habari katika kongamano la saba la wadau wa afya nchini( Tanzania
Health Summit).
Aidha amesema kuwa lengo la mradi
huo ni kutekeleza miradi ambayo italeta matokeo chanya na kuonekana
katika jamii na unafanya uboreshaji katika mfumo wa afya, mfumo wa
fedha, mfumo wa vifaa tiba, na mfumo wa upatikanaji wa dawa.
Mfano wa mifumo hiyo ni pamoja na CHF iliyoboreshwa mfumo wa upatikanaji wa dawa (Jazia PVS)na Mradi huu upo hapa katika maonesho ili kuchangia tija katika masuala mazima ya mfumo wa afya nchini, kuchangia mifumo ya afya nchini, pamoja na kujifunza.
Ally Abdallah.
“Kwa kuwa kila tunachokifanya lazima kilete
matokeo kwahiyo sisi tupo hapa ili kuonesha miradi tuliyoifanya na si
vinginevyo” amesema Abdallah
Amesema Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS,) ni
mradi mkubwa na wenye mafanikio kwani upo hadi kwenye ilani
inayozungumzia upatikanaji wa dawa nchini.
Hata hivyo Abdallah amesema wao wamejipanga
kuendelea kutoa elimu katika banda lao kwenye kongamano hilo
la saba la wadau wa afya kwani kupitia wadau hao ndipo wanapopata
fursa zaidi ya kuutangaza mradi na kujitangaza kwa jamii kwa ujumla.
0 Comments