WABUNGE 19 VITI MAALUMU WA CHADEMA WAAPISHWA BUNGENI DODOMA




📌HAMIDA RAMADHANI


WABUNGE 19 Wa viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wameaapishwa kuwa wabunge rasmi leo jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wabunge hao spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joab Ndugai amesema ibara ya 78  ibara ndogo ya kwanza inavitaka vyama siasa kuteua wabunge wa viti maalumu kuwakilisha chama.

"kama inavyofahamika nchi yetu ilikua na uchaguzi Mkuu October 28 ambapo kikanuni vyama vya siasa vikivyokidhi vigezo viteue wabunge viti maalumu na kwa upande wa chama cha chadema kilikidhi vigezo vya kuwepo kwa wabunge wa viti Maalumu chadema"amesema Ndugai.

Katika ibara ya 68 inasema kuwa kila mbunge aapishwe mbele ya spika wa bunge na siyo kwenye ukumbi wa bunge kama watu wanavyodhani,na kiapo hiki ni kiapo aminifu ambacho mbunge anatakiwa aape kabla hajaanza shughuli za bunge


Spika Ndugai.

Aidha amesema kwa kitendo cha kuwaapisha wabunge hao  atatoa taarifa February 2  2021 katika  ukumbi wa bunge .

Pia Spika Ndugai amewatoa hofu wabunge hao kwamba wasijione wanyonge kwa uchache wao bungeni kwani atatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weledi.

Kwa upande wake Halima Mdee akiongea kwa niaba ya wenzake mara baada ya kula kiapo amesema kuapishwa kwao siyo hisani bali chama chao kilikidhi vigezo na ni sehemu ya ushindi wa chama chao.

"Mimi pamoja na wenzangu tutafanya kazi kwa ushirikiano kama kambi rasmi ya upinzani bungeni hivyo wanachama na Wananchi wasiwe na hofu  kwani tunaenda kufanya kazi tukiyoagizwa"

Nitafanya kazi kama kawaida Spika tushafanya kazi ndani ya miaka kumi na kuna vijana wapya sisi kama dada zao tutawaongoza watafanya kazi vyema kwa mwendo wetu ule ule.

Halima Mdee.

 Pia Mdee alikishukuru chama Chao cha Chadema kupitia  mwenyekiti wao Freeman Mbowe kwa kuwaamini kuwapa nafasi ya kuwawakilisha bungeni.

 Hata hivyo wabunge hao 19  walioapishwa ni  pamoja na Halima Mdee,Grace Tendega,Ester Matiko,Secilia Pareso,Ester Bulaya,Agnesta kaiza Nusrat Hanje,Ester kishoa,Hawa Mwaifunga,Tunza malopo,Asia Mohamed,Felister Njau, Nangejwa Kabonyoka,Sophia Mwakagenda,Kunti Majala, Stellah Mviao,Anatopias Rwikila,Salome Makamba, conchestar Rwamlaza.

 


Post a Comment

0 Comments