ELIMU KWA NJIA YA TELEVISION MSAADA KWA WANAFUNZI KIPINDI CHA CORONA?




 ðŸ“ŒNOEL STEPHEN

UGONJWA wa COVID 19 ni ugonjwa  wa kuambukizwa ambao unatajwa kuwa miongoni mwa magonjwa ya mlipuko  unaosababishwa na virus vya  corana.

Virusi  hivyo  vipya  havikuwa vikafamika  hapo awali na  sayansi ya tiba , Corona ni kirusi kinachosababisha  maradhi  kwa wanayama na bidamau pia  hasa kwa kushambulia katika njia ya hewa na mfumo wa upumuaji .

Mara baada ya Waziri  waziri wa  Afya Mhe Ummy Mwalimu kumtangaza mgonjwa wa kwanza   wa ugonjwa wa COVID 19  mnamo mwezi Maachi mwaka huu ,jamii ilianza kupata shaka  na kuingiwa na wasiwasi  na hofu kubwa juu ya kuweza kuukabili ugonjwa huu.

Kufuatia hali hiyo Serikali kupitia waziri mkuu Mhe Kasim Majaliwa alikuja na tamko juu ya kujikinga na  ugonjwa huo ikiwemo kunawa mikono,  kutumia  barakoa  katika sehemu zote za mikusanyiko  na katika sehemu za huduma kama hospitalini  shuleni , mahakamani na sehemu zingine zote ikiwemo kutenga maeneo ya kuwahifadhi waliokwisha ambukizwa ugonjwa huo(karantini).

Aidha  Waziri Mkuu alitangaza kufugwa kwa shule zote za seikali na binafsi    kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Machi 17 2020 .

Baada ya tangazo hilo kutoka kwa Serikali,swali kubwa lilikuwa ni juu ya mustakabari wa elimu hususani kwa wanafunzi waliokuwa kwenye madarasa ya mtihani.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu walijifungia kuumizwa kichwa na wakaja na jibu la namna bora ya wanafunzi kuendelea na masomo katika kipindi ambacho nchini ipo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

 Na jawabu likawa moja tu; wanafunzi kufuatilia vipindi vya masomo  kwa kutumia vyombo vya habari kama radio ,luninga na simu  mfumo huo ambao ulikuwa rafiki kwa wanafunzi wa mijini na wanao miliki vyombo hivyo.

Hii ni hatua njema kabisa katika ukombozi wa elimu katika kipindi kigumu cha mpito,lakini swali kubwa likawa je;njia hiyo ilikuwa msaada kwa wanafunzi wote nchini?

 Ester Mwahisi mkazi wa  Kata ya Mazae katika Wilaya ya Mpwapa anasema kuwa  kutokana familia yake kushidwa kumiliki simu ambayo inaweza Kutumia mtandao na kutokuwa na Runinga wala radio  watoto wake hawakuweza  wake kufuatilia vipindi hivyo.

Hali ya kipato kwa baadhi ya wazazi katika maeneo mbalimbali nchini kiliwanyima fursa baadhi ya  wanafunzi kupata elimu hiyo ambayo ilikuwa inatolewa katika muda sawa na ule wa shule.

Kwa upande wake Charles Jonson ambaye ni  Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Idilo iliyop Wilaya ya Mpwapwa amesem kufungwa kwa shule katika kipindi cha Corona  kuliwaathiri wanafunzi  katika maeneo hayo ya vijijini hususani wale waliokuwa kwenye madarasa ya mitihani wakiwemo  darasa la Nne na darasa la Saba.

Tulipo fungua tu tulijaribu kuwaliuza wanafunzi wangapi walikuwa wanafuatilia masomo kwa njia ya televisheni kati ya wanafunzi  48 ni wanafunzi  7 tu ndio walikuwawakifuatilia lakini nao sio hadi mwisho walifuatilia mwanzoni tu  baadae wakaacha  kufuatilia.

Charles Jonson

Jonson amesema mara walipofungua shule tu waliandika mtihani wakujipima ambapo amesema hakuna mwanafunzi aliye pata daraja la kwanza.Amesema lengo la mtihiani huo ni kupima wanafunzi hao kama wanakumbuka chochote walichofundishwa katika kipindi hicho walipokuwa kwenye mapumziko ya lazima.
 Mwalimu Jonson amesema ni wanafunzi wachache tu ndio  walipata alama B na wengi walipata alama C wakati kabla shule hazijafungwa Hapo tarehe 17 Machi watoto wengi walikuwa kwenye daraja A hivyo walitoa mtihani huo ili kuweza kujua waanzie wapi kuziba mapengo ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Kwa upande wake Mery Chakupewa  afisa Elimu Msingi  Wilaya ya Mpwapwa amekiri kuwa mfumo wa usomaji kwa kwa njia ya mitandao imewasaidia baadhi ya watoto na hivyo haikuweza kuwadaidia watoto wote hasa waishio vijijini.

Mwl.Chakupewa amesema serikali kupitia wizara husika  ya Uchukuzi na Mawasiliano lazima iweze kuboresha mifumo hiyo kipindi kingine kama likitokea janga kama la CORONA linaloweza kusababisha shule kufungwa kuweza kuwajumuisha hata Watoto wa vijini.

Amesema japo kuwa serikali imefanya kazi kubwa kajaribu kusambaza umeme katika vijiji vingi hapa nchini kwa kupitia mradi wa Wakala waUmeme vijijini (REA) lakini baadhi familia zimeshidwa kuunganishaa umeme huo kwenye nyumba zao ili kuweza kunufaika na fursa za Serikali kama hizo kutokana na uduni wa maisha yao.

Aidha amedai  kuwa pia kuna wakati wa kipindi cha CORONA baadhi ya Wazazi walikuwa wakiwatumia Watoto hao katikati kazi mbali mbali kama za kuuza biashara ndogo ndogo hivyo ulikosekana muda wa kusoma kwa watoto hao.

Wakati watoto wengine wakiwa kwenye runinga wakijifunza,wazazi wengine walitumia muda huo kutumikisha watoto wao kuwasaidia kuuza biashara zao.

Mery Chakupewa  

Naye mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri amesema katikati kipindi cha likizo ya Corona kama wilaya kupitia Idara husika waliweza kutoa maelekezo na Elimu kupitia makanisani na misikitini namna bora ya Wazazi kuwasaidia Watoto wao kujifunza wakati  wa kipindi hicho cha mpito.

Bila Shaka madhara lazima yawepo kutokana na mwamko mdogo Wa baadhi ya wazazi, lakini umaskini wa kipato kwa baadhi ya familia hivyo haikwepeki

Jabir Shekimweri

 

Post a Comment

0 Comments