JESHI LA POLISI DODOMA, LANASA SILAHA ZINAZOTUMIKA KWA UHALIFU/ASKARI ZAIDI YA 300 KUFANYA DORIA SIKUKUU ZA CHRISMASS.

 


JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za unyang’anyi  wa kutumia silaha baada ya kupatikana wakiwa na Bunduki  mbili aina ya Shotgun zilizotengenezwa kienyeji mfano wa pisto pamoja na risasi tano za bunduki aina hiyo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kukamata watuhumiwa hao baada ya kufanya oparasheni mbalimbali kwakushirikiana na Jeshila Polisi Mkoa wa Morogoro ambapo mnamo Desemba 23 Mwaka huu maeneo ya Chalinze nyama Wilayani Chamwino Michael John alikutwa na risasi tano za shotgun wakijiandaa kufanya unyang”anyi baada ya kuhojiwa alikiri na kuwataja wenzake.

 

Aidha,Kamanda Muroto amesema kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakifanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma na Morogoro ambapo Disemba 19 mwaka huu walifanya uhalifu Kijii cha Izava baada ya  kuvamia  Duka na kumjeruhi mwenye duka  kwa risasi na kupora fedha kiasi cha Sh milioni30 na simu 40.

Kamanda Muroto amesema kuwa wamewakamata watuhumiwa saba ambao ni wakazi wa Dodoma  baada ya kukutwa na vifaa mbalimbali ambavyo  vizaniwazo kuwa ni za wizi  zikiwemo kompyuta,televisheni printer na muziki sistimu.

 

Katika hayua nyingine kuelekea Sikukuu ya Krismas Kamanda Muroto amesema Jeshi limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao ikiwa ni pamoja na kutoa elimu katika nyumba za ibada ili watu washerehekee kwa amani ambapo  linashirikiana na jumla ya vijana300 kama ulinzi shirikishi  amesema madereva wanaobunja sherrtia za usalama baearabarani watawachukulia hatua za Kisheria.

 

 

Post a Comment

0 Comments