JESHI LAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS JOHN MAGUFULI.

šŸ“ŒHAPPINESS MTWEVE.

KATIKA kutekeleza maagizo ya Rais, Dk.John Magufuli ya kuimarisha mazao ya kimkakati Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wameanza kutekeleza agizo hilo kwa vitendo kwa kuanza kuzalisha Miche bora ya mikorosho huku wakitarajia kulima hekari 2000 za zao hilo.

Pia limesema liko tayari kuzalisha miche bora ya mikorosho katika mikoa yote 17 ya Tanzania ambayo imetajwa kuwa na uwezo wa kulima zao hilo.

Kaimu Kamanda wa kikosi cha Jeshi 834 Makutupora, Luteni Kanali, Festo Mbaga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo, amesema mkakati wa JKT ni kuhakikisha agizo la Rais Magufuli kufikisha tani milioni1 ifikapo 2025 linafikiwa na kwa sasa nchi inazalisha korosho tani 315,000 na mashamba makubwa yapo mikoa ya kusini.

Mbaga amesema wameamua kuwekeza nguvu kubwa katika mikoa iliyotajwa kuwa na uwezo wa kuzalisha korosho ikiwemo Singida na wanafanya kazi hiyo kwa kushirikisha vikosi mbalimbali na wataalamu.

Ametoa wito kwa wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa wilaya na mikoa kwenye mikoa 17 ambayo utafiti ulionesha wanaweza kulima korosho kushirikiana na JKT ili tuweze kushirikiana nasi tuwazalishie mbegu bora na za uhakika.

ili kuunga mkono uimarishaji wa mazao ya kimkakati, ikiwemo zao za korosho JKT tutahakikisha tunazalisha mbegu za kutosha na bora na wananchi wanapata kwa gharama nafuu, mafano hapa tunauza mche mmoja kwa shilingi 1,000,amesema.

Akizungumza mradi kitalu cha miche ya kikorosho ya kisasa inayozalishwa JKT Mkiwa wilayani Manyoni kwa ushirikiano wa 834 kikosi cha Jeshi Makutupora na 843 kikosi cha Jeshi Nachingwea,  Kaimu Kamanda wa kikosi cha Jeshi 834 Makutupora, Luteni Kanali, amesema wamezalisha miche 300,000.

Amesema katika kiasi hicho, miche 7,500 JKT itaipanda kwenye ekari 250 za shamba lao, huku miche 100,000 inakwenda kwenye mradi  wa korosho, miche 50,000 ikilelekwa Ikugi na inayobaki watauziwa mwananchi mmoja mmoja.


Mbaga amefafanua kuwa lengo lao ni kulima ekari 2,000 za korosho, mwaka jana walipanda miche 7,500 katika ekari 250 na msimu huu watapanda idadi hiyo hiyo ili kufikisha ekari 500 katika kuelekea mkakati wao wa kufikishia ekari 2,000.

Naye Msimamizi wa mradi wa kuzalisha mbegu za korosho kutoka Nachingwea Luteni Kanali Nyagali Malecela amesema wanaweza kufikia azima ya serikali kwa kuzalisha mbegu bora, hivyo akiwataka wananchi kuhangamkie fursa hiyo.

Akizungumzia Kikosi cha Jeshi 843KJ  Nachingwea amesema walianza uzalishaji wa mbegu za miche ya korosho mwaka 2016 ambapo walianza kwa kuzalisha miche 100,000 na mwaka 2017 walizalisha miche 190,000 na 2018 miche 200,000 ilizalishwa.

Pia  Malecela amesema JKT kutumia nguvu kazi ya vijana wa kujitokea kunafanya mbengu wanazozalisha kuwa na bei nafuu.

Naye mkulima wa Mkiwa Mniru Selemani aliyenunua miche 4,000 alipongeza hatua ya JKT ya kuzalisha miche ya mbegu kwani itasaidia kuondoa changamoto ya mbegu.

Wananchi tumehamasika sana na kilimo hiki, Ila changamoto ilikuwa ni uhaba wa mbegu, mimi mwaka jana niliandaa ekari 300 lakini kutokana na tatizo hilo nikapanda mwaka jana ekari 100, na kwa miche hii niliyochukumuj matarajia kwenda kupande kwenye ekari 200 zilizobaki, nawasukuru Sana JKT, amesema.

Kwa upande wake Ofisa ugani kutoka 834KJ, Kapteni Ezekiel Mtani ameeleza kuwa kupitia mradi huo JKT inazalisha mbegu bora zinazoanza kuzaa baada ya miaka mitatu zikiwa zimetoka kituo cha utafiti cha Naliendele cha Mtwara

" Uzalishaji wa miche ya mbegu ya korosho kunahitaji umakini na usimamizi wa karibu, huku ukitumia udogo ambao haujawahi limwa na kuwa na uwiano sahihi wa mbolea ya samadi na udongo ambao Ardhi yake haijawahi kulimwa, hivyo kwa kuwa JKT imesheheni wataalamu wa ugani umewarahisishia kuzalisha mbegu bora, amesema.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments