KUPUNGUA KWA BEI ZA BIDHAA,KUMESABABISHA MFUMUKO WA BEI KUSHUKA HADI 3.0 %

 

                                Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ruth Minja.

📌HAMIDA RAMADHANI 

 MFUMUKO wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba,2020 umepungua hadi kufikia 3.0 kutoka asilimia 3.1 kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba ,2020.

 Akiongea na waandishi wa habari leo jijini hapa Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ruth Minja amesema hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko  ya Bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba,2020 umepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2020.

 Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2020 umechangiwa hasa na kupungua kwa bei za baadhi  ya bidhaa za vyakula kwa kipindi Kilichoishia mwezi Novemba,2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Novemba,2019.

 

"Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei kwa mwezi Novemba,2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Novemba,2019 nipa moja na Mchele asilimia 4.5, Mahindi asilimia 14.3,Unga wa Mahindi asilimia 5.7,Unga wa Mtama asilimia 4.4,Viazi vitamiu asilimia 2.6, vyakula vya Watoto( Lishe) asilimia1.8 na Ndizi za kupika asilimia 4.9. Ruth Minja.

Ameongeza kuwa mfumoko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa mwezi Novemba,2020 umepungua hadi asilimia 2.8 kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2020",amesema.

 HALI YA MFUMOKO WA BEI NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI.

 Amesema Nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba,2020 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.46 kutoka asilimia 4.84 kea mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2020.

 Kwa Upande wa nchi ya Uganda, Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba,2020 umepungua  hadi kufikia asilimia 3.7 kutoka asilimia 4.5 kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba,2020.

Post a Comment

0 Comments