MKUU WA POLISI APEWA MAAGIZO, HAKIKISHA MKESHA NA SHEREHE ZA CHRISMASS ZINAFANYIKA KWA AMANI NA UTULIVU.

 



📌BARNABA KISENGI.

MKUU wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri  amemuagiza Mkuu wa Police Mpwapwa Cosmas Mboya kuhakikisha katika mkesha wa sikukuu ya Xmas's hali ya ulinzi na usalama inaimarika katika makanisa na majumbani ili waumini wafanye ibada kwa usalama na amani na watakao kuwa majumbani wawe katika hali ya usalama wilayani hapo. 

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mahojiano maalumu na mwandishi wa CPC  blog Barnabas kisengi wilayani hapo katika kuelekea mkesha wa ibada ya Xmas's na sikukuu yenyewe ya Xmas's.

"Nimemwagiza mkuu wa police kuhakikisha suala la ulinzi linaimarika ili wananchi washerekee sikukuu kwa utulivu na amani hivyo ajipange na askari wake kuhakikisha wanapitia maeneo ya Nyumba za ibada kuhakikisha suala la ulinzi linaimarika kwa kuwashirikisha wenyeviti wa Mitaa,vijiji na vitongoji huku wakishirikiana na Jeshi la akiba na vikundi vya ulinzi shirikishi"amesema shekimweri

Shekimweri ametoa tahadhari kwa waalifu wote kuwa hawata pata nafasi ya kufanya uhalifu katika kipindi hichi cha sikukuu kwakuwa serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri kusimamia ulinzi na usalama na mali za wananchi katika kipindi hichi. 

Kwaupande wake mkuu wa police wilaya ya mpwapwa Cosmas Mboya amesema wao wamejipanga vizuri kuimarisha ulinzi na usalama katika mkesha wa ibada ya Xmas's katika makanisa na maeneo Mengine ya starehe na majumbani kwa kipindi chote cha sikukuu ya Xmas's na mwaka mpya 2021.

"Nikuhakikishie tumejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi na jeshi la akiba kwa kuwashirikisha viongozi hasa wenyeviti wa Mitaa,vijiji na vitongoji hivyo tunaamini hali ya usalama itakuwa shwari na nitoe onyo kwa wale wenye nia ya kuleta uhalifu katika kipindi hichi cha sikukuu watapata tabu sana" amesema mboya

Katika kuelekea sikuku ya Xmas's na mwaka mpya kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya mpwapwa imejipanga kuhakikisha inaimarisha hali ya ulinzi na usalama imeimarika kwa wananchi wa wilaya ya mpwapwa kwa usimamizi wa mkuu wa wilaya ya mpwapwa.

Mwisho

 

Post a Comment

0 Comments