MSEMAJI WA SERIKALI , DKT:HASSAN ABAS ASEMA HAJAPOKEA BARUA KUTOKA KWA WAKIMBIZI WA BURUNDI..


 ðŸ“ŒBBC

WAWAKILISHI wa wakimbizi wa Burundi nchini  wameandika barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Guterres na Kamishna Mkuu wa umoja huo anayeshughulikia Wakimbizi Grandi kuomba makazi katika nchi nyingine.

Barua hiyo imesema kuwa baadhi ya wakimbizi wananyanyaswa na kurejeshwa kwao bila kufuata utaratibu maalum ndio maana wanaomba taifa lingine liweze kuwapokea.

Lakini mwanzoni mwa mwezi huu shirika la kutetea haki za binadamu Human Watch, ilitoa ripoti ya kukemea jambo hilo la kuwa Tanzania inawanyanyasa wakimbizi na kulitaka taifa hilo liwalinde kwa kufuata sheria za kimataifa.

Wakimbizi hao wanasema kuwa wameambiwa kuwa wanapaswa kurudi kwao kwa sababu sasa hivi taifa la Burundi liko salama.

Hata hivyo hapo nyuma, serikali ya Burundi na Tanzania zilifikia makubaliano ya wakimbizi kurudi nyumbani kwa kuwa kuna amani kwa sasa ingawa wakimbizi wenyewe wanasema, si serikali yoyote kati ya hizo mbili ndio wana haki ya kusema usalama upo au haupo.

Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania , Dkt Hassan Abas alisema hawajapokea barua yeyote kutoka kwa wakimbizi, "kama kuna changamoto yeyote kwenye usimamizi wa wakimbizi Tanzania kuna ofisi za shirika la umoja mataifa linalosimamia haki za wakimbizi, serikali ipo ,hizo changamoto tungeletewa na kuzitatua".

Aliongeza kusema "Tunachokisisitiza kuwa Tanzania haiwezi kuwatesa wakimbizi , Tanzania haiwezi kumdhuru mkimbizi, ambaye sisi wenyewe ndio tulimkubali, tungeweza kumkataa lakini tumemkubali na akapata kinga ya kimataifa ya kukaa nchini kwetu mpaka itakaporejea kuwa na amani, sasa tunashiriki vipi kumuhujumu."


Post a Comment

0 Comments