MSICHOME MATAIRI WALA KUPIGA FATAKI.

 


📌BARNABA KISENGI.

Mwenyekiti wa mtaa wa chinyoyo Kata ya kilimani jijini Dodoma Faustina Bendera amewataka wananchi wa mtaa wa chinyoyo kuelekea sikukuu ya kumaliza mwaka na kuingia mwaka mpya washerekee kwa amani na wajihadhari katika mkesha wa mwaka mpya kutochoma matairi na kupiga fataki katika mkesha huo. 

alikuwa akizungumza katika mahojiano maalum na mtandao huu mapema leo .

 "Najua tunapokuwa na sherehe za mwaka mpya maeneo mengi wananchi wamekuwa wanatabia ya kuchoma matairi moto na kupiga mafataki ovyo hilo ni kosa na hivyo nawatadharisha wananchi wa mtaa wangu wasijihusishe na vitendo hivyo watakuwa wamefanya kosa kinyume na sheria za nchi Kama hawana kibali kutoka jeshi la police na watakao kafanya hivyo watachukuliwa sheria kali"amesema Faustina 

Pia amewakumbusha wananchi wa mtaa huo kuwa baada ya sikukuu hizi mbili watambue kuwa shule zitafunguliwa hivyo kunamaandalizi ya watoto kwenda shule hivyo lazima wawaandae watoto wao mapema kwa maandalizi ya shule

"Na kwa wale wazazi ambao watawaficha watoto wao kutokwenda shule nitawachukulia hatua kali za kisheria maana Kuna tabia ya wazazi kuwazuia na kuwaficha watoto wasiende shule bila sababu wajue tutawashulikia maana serikali ya awamu ya tano imetoa elimu bila malipo hivyo hakuna Sababu ya kutawapeleka watoto shule"amesema Faustina

 Ametoa wito kwa wananchi wanaojihusha na kilimo watumie muda huu kulima na kupanda kwa kwa kuwatumia maafisa kilimo katika mashamba yao ili waweze kujikwamua kiuchumi. 

 Mwisho

 

 

Post a Comment

0 Comments