WAZIRI MKUU MSTAAFU, AMEWATAKA WATAALAM KUANGALIA HISTORIA YA KILIMO.

 


📌NA NAZA KIRIMBO.

 WAZIRI  Mkuu Mustaafu Mizengo Pinda amewataka wataalamu wa masuala ya kilimo nchini kuangalia historia ya kilimo ili kubaini ni mazao gani yalikuwa yalifanya vizuri ikiwamo ngano ili kutafuta namna ya kuirudisha katika hali ya awali.

Pinda ameyasema hayo jijini hapa wakati wa mkutano wa Shirikisho la Wachumi Kilimo Tanzania (Agrest) uliokuwa na lengo la kujadili namna ambavyo kilimo kinavyoweza kukuzwa na kuendelezwa ili kiweze kuchangia kuondoa umasikini kwa Taifa la Tanzania na dunia kwa ujumla.

Amesema kuna baadhi ya changamoto ambazo wataalamu hao wanatakiwa kuzifanyia kazi kama vile kuangalia historia, ni wapi palikuwa na nguvu kubwa ya uzalishaji na kwanini nguvu hiyo ilipotea ili kutafuta namna ya kuirudisha.

Amesema katika kipindi cha nyumba zao la ngano lilikuwa likIfanya vizuri nchini Tanzania lakini kwa sasa malighafi hiyo inaagizwa kutoka nje ya nchi jambo ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho ya pekee.

Kuna taarifa kidogo inanikere kera, mfano ni kwa nini Tanzania tuendelee kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi wakati tunaweza kuzalisha michikichi, alizeti na mazao mengine tukapata mafuta ya kutosha,  kwa nini tuagize sukari kutoka nje ili hali tuna ardhi kubwa ya kutosha, hali nzuri ya hewa, mvua ya kutosha ambayo inaweza kuzalisha sukari hadi tukauza nje ya nchi,. 

Mizengo Pinda.

Amesema wataalamu wanatakiwa kukaa chini na kutoa elimu ya kutosha ili kuona ni aina gani ya ng’ombe wa kufuga na kwa kiwango gani, kwa ubora gani ili tuweza kupata kiwango cha maziwa chenye utoshelezi.

Aidha amesema ni wakati muafaka kwa Bara la Afrika kufanya kila jitihada kuhakikisha linajitosheleza katika kujiuzia bidhaa zinazotokana na mazao mbalimbali ya chakula badala ya kutegemea vyakula vinavyotoka nje.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Agrest Elibariki Msuya alisema mkutano huo unalenga kuangalia mifumo ya uzalishaji na usambazaji wa chakula Tanzania na duniani ili kuleta tija katika sekta ya kilimo.

Hata hivyo amesema licha ya kuwa kuna Tanzania kuna viwanda vingi vinavyozalisha bidhaa za ngano lakini moja ya mikakati watakayoiweka ni ya kuongeza viwanda hivyo ili vizalishe kulingana na mahitaji.

“Ili kuweza kutumia bidhaa zetu za ndani ni lazima tulinde viwanda vinavyozalisha bidhaa hapa nchini kwa kusimamia sheria zetu na ndio maana Serikali iliongeza tozo kidogo kwa bidhaa za kutoka nje ili kuongeza ulaji wa bidhaa za viwandani, hapo tutakuwa tumeongeza tija,” alisema Msuya

 

Post a Comment

0 Comments