NI FUNGA MWAKA! KAMBI YA MAKAPERA CPC YAPATA PIGO...

 


📌MWANDISHI WETU

Kambi ya makapera ndani ya Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma (CPC) imepata pigo baada ya kukimbiwa na wafuasi wake wawili.

Alex Sonna (Mtandao wa Full Shangwe) na Agusta Njoji (Gazeti la Nipashe) mwishoni mwa juma (12/12/2020) wameamua kuhama kambi hiyo baada ya kufunga Ndoa Takatifu katika Kanisa  Katoliki parokia ya Nkuhungu na baadaye kujumuika na ndugu,jamaa na marafiki katika sherehe ya kuwapongeza wawili hao katika ukumbi wa LAND MARK uliopo eneo la Kilimani jijini Dodoma.



Alex na Agusta wote ni wanachama hai na watiifu wa CPC,hivyo klabu ilikuwa mbele katika kuhakikisha lengo la wanachama wake linatimia.




Mbali na waandishi wa Habari wa Jiji la Dodoma, sherehe hiyo pia imeudhuriwa na wageni wa kada mbalimbali kutoka katika taasisi za Serikali na binafsi.









Post a Comment

0 Comments