RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MAAGIZO WATUMISHI WOTE KUMALIZA KUJAZA FOMU ZA MAADILI KABLA YA TAREHE 30,DISEMBA,2020

 

📌FAUSTINE GIMU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli  leo Disemba 24,2020 amemwapisha  kamishna wa Maadili  Jaji Sivangilwa Mwangesi huku akitoa maagizo kwa watumishi wote kuhakikisha  wanakamilisha kujaza fomu za maadili ya utumishi wa umma kabla ya tarehe 30,Disemba ,2020.

Akizungumza mara baada ya uapisho huo uliofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa ifikapo Disemba 30,2020 watumishi wote wahakikishe wanakamilisha kujaza fomu kabla ya Tarehe ,30,2020.

Niwaombe wafanyakazi wenzangu ambao ambao wana wajibu kujaza hizi fomu mhakikishe mnajaza kabla ya Tarehe 30,Disemba,2020 ili zimfikie kamishna mpya kwa sababu sasa hakuna tena sababu ya kisingizio nimejua wengi hatujapeleka fomu hata mimi hapa sijapeleka  fomu sasa nitaijaza harakaharaka ili niweze kukufikishi a hizo fomu kwa taratibu za nchi
 amesema.

Aidha,Rais Dkt.Magufuli ametoa maagizo kwa tume ya Maadili kuacha kurudisha fomu kwa njia ya mtandao  ili kuepuka wahalifu wa mtandao wanaoweza kughushi na kuleta mtafaruko.

Nilimweleza Marehemu  na tulikuwa tumekubaliana  kwamba fomu unaweza kuzidownload kwenye mtandao lakini ukishazijaza usirudishe tena kwenye mfumo wa mtandao mtu akishajua ile program anaweza kuedit [kuhariri]na hapa wapo wengi umejaza milioni 10 mtu anakuja kukujazia milioni 100 halafu wewe unakuja kuulizwa ulijaza milioni 100 hapa na originality inapotea msikubali kamwe kurudisha fomu kwa njia ya mtandao  
amesema.

 Kamishna wa maadili     Sivangilwa Mwangesi ameahidi kutekeleza majukumu yote aliyopewa kwa kufuata miongozo ya nchi.

Akitoa Salam za pongezi,Naibu katibu mkuu Wizara ya katiba ba Sheria Amon Mpanju ameomba mhimili wa Mahakama kuongezewa nguvu  kwa kuongeza majaji  huku Naibu Waziri wa Menejimenti  ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi  amebainisha kuwa  mpaka sasa karibia asilimia 92 ya watumishi wa umma wanajaza fomu za utumishi wa umma na kutaja mali zao.

 Ikumbukwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Sivangilwa Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili kuanzia  Tarehe 23 Disemba 2020 ambapo  Jaji Mwangesi anachukua nafasi ya Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Harold Nsekela aliyefariki Dunia hivi Karibuni.

MWISHO.

 

 

Post a Comment

0 Comments