📌HAMIDA RAMADHANI
IMEELEZWA kuwa kundi la Vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi umri wa miaka 24 ndilo kundi linalopata maambukizi kwa kasi kubwa nchini.
Akiongea katika maadhimisho ya siku
ya UKIMWI Duniani kimkoa yaliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square katibu
Tawala Dodoma Keissy Maduka amesema takwimu zinaonyesha kuwa
asilimia 44 la kundi la Vijana lipo kwenye hali hatarishi ya kupata maambukizi ya virus vya Ukimwi na Ukimwi.
Katibu Tawala huyo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amesema katika kipindi cha miaka ya 2012 hadi 2014 Mkoa wa Dodoma ulikuwa ni miongoni mwa mikoa yenye maambukizi madogo kwa asilimi 2.4.
"Sasa tumeweza kuona takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaonyesha kuwa hali ibadilika ambapo kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2017 hali ya maambukizi mkoa wa Dodoma ni asilimia 5 hivyo Dodoma yetu imeweza kuingia kwenye mikoa hatarishi hakika hili ni tatizo kubwa hasa kwa Vijana wetu,"amisema Katibu Tawala Maduka.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika siku hiyo kujitokeza kwa wingi kwakupima na kutambua afya zao Mapema na kuacha uoga wa kujua afya zao kuwa kigezo cha kuhofia kufa Mapema.
Kila mmoja wetu ampime atambue afya yake kwani ukipima na ukijitambua mapema kama unamaambukizi ya virus vya Ukimwi unanafasi ya kuishi vizuri kea amani na furaha.
Keissy Maduka
Kwa Upande wake mratibu wa Ukimwi mkoa wa Dodoma kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Abdih Ahmed amesema visababishi vya Ukimwi havitofautiani na vinginekatika bara la Afrika kuwa na wapenzi wengi,ngono zembe,kuchagia vitu vyenye ncha kali na hata ukatili wa kijinsia.
Amesema visababishi hivyo vimechangia ongezeko kubwa la Vijana kuwa na maambukizi na kuwa na idadi kubwa la watoto yatima .
Takwimu kutoka NBS zinaonesha kuwa kuanzia mwaka 2017 Dodoma ilikuwa asilimia 5 ya maambukizi tofauti na mwaka 2013 mpaka 2014 hali ya maambukizi ilikuwa 2.9 hivyo Hali ya maambukizi Dodoma imeongezeka
Abdih Ahmed
Akitoa ujumbe,mwakilishi kutoka TACADS Yeriko Kawanga amesema ukimwi bado ni tishio .
"Kwa mujibu wa takwimu zilizopo katika kila watu 100,watu wanne wana maambukizi ,hili janga la Taifa." Amesema
Amewataka wananchi waendelee kyjitojeza kupima Afya zao ili waanze kupatiwa tiba mapema.
Naye Annamary Oscar kutoka konga Nacopha baraza la Vijana wanaishi na virus vya Ukimwi mkoa wa Dodoma amesema Furaha yao nikuona wamefanikiwa kuwarudisha jumla ya Vijana 122 kwa mwaka 2019 hadi 2020 waliokatisha matumizi ya dawa za kufubaza makali ya virus vya Ukimwi na Ukimwi ARVS.
Amesema kwa Upande wake pamoja na
Vijana wengine wanaojitambua kuwa na virusi vya Ukimwi wamekuwa na afya zilizoimarika
kwa kuendelea kutumia dawa hizo za kufubaza virusi vya Ukimwi ARVS.
Wasanii wakitoa burudani... |
0 Comments