VIJANA, MWAKA UJAO UWE WA MABADILIKO CHANYA.




📌DEVOTHA SONGORWA.

VIJANA nchini wametakiwa kusimamia malengo yao kwa kutumia vyema nguvu walizo nazo kwa mustakabli wa Taifa kwa ujumla badala ya kuogopa changamoto.

 Hayo yamesemwa  na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Taifa  kupitia  Chama Cha Mapinduizi (UVCCM),Raymond Mwangwala wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake kuhusu namna watakavyomuenzi aliyewahi kuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM,Egla Mamoto aliyefariki dunia Disemba 27 mwaka huu.

 Alisema vijana wengi wamekuwa wamekuwa wakikata tamaa katika safari yao ya kusaka mafanikio akiwataka kutumia mwaka 2021 kuwa na mabadiliko kwa kusimama imara na kutokukubali kushindwa wala kuyumba kuhakikisha wanakuwa na mchango kwa nchi.

 "Cha kumuenzi ni katika maandiko aliyoyaacha na kama umoja wa vijana ni kuenzi mambo ya Egla utu,upambanaji vijana wengi wakishindwa kidogo tu wanarudi nyuma anaanza kutukana kumbe inatakiwa utulie, simama jipukute vumbi endelea na safari no retreat no salenderna kusimama katika yale wanayoamini yana mchango kwa Taifa",alisema Katibu Mkuu huyo.

 Akizungumzia mchango wake katika Chama alisema amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinapata ushindi katika uchaguzi wowote ule   na kusimamia katika yale aliyoyaamini kwa kutumia vipaji alivyojaaliwa wakati wote wa uhai wake akisema   wamepata funzo kubwa.

 “Kabla ya umauti kumfika mpaka saa nne usiku alikuwa akichat katika makundi ya whatsAspp akiwatakia watu kheri ya mwaka mpya tumejifunza tuwe tayari wakati wote, tunaweza kuwa na mipango yetu lakini Mungu naye ana mipango yake  kwahiyo tuwe na upendo na ushirikiano tujijenge kwa watu social capital ni kubwa kuliko kujidai na kujiona wewe ni zaidi yaw engine",alieleza Mwangwala.

 Kuhusu mchango wake katika nafasi ya uongozi kama mwanamke aliwataka wanawake kuiga mfano huo kwa kuonyesha utuhubutu kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi akisema hakuna maendeleo katika Tiafa lolote yasiyomtaja mwananmke.

“Kama mwanamke alionyesha kwamba wanamke anaweza bila   kuwezeshwa aligombea nafazi zinazohusu wanaume alishinda, alifanya kazi zinazohusu wananume alifanya vizuri aligombea nafasi za wanawake aliperform vizuri alionyesha wanawake tusibaki nyuma tusisubiri kubebwa tusimame maana wanawake wakisamam watasaidia nchi yao", alisisitiza Katibu Mkuu.

Aidha alihitimisha kwa kuwataka wanaume kutambua uwezo wa wanawake na kuwatia moyo pindi wanapoonyesha nia ya  kufanya jambo fulani la kimaendeleo na kuondokana na mtazamo hasi kuhusu kundi hilo huku akiwataka wazazi kukuza vipaji vya watoto wao kwa kike na siyo kuwakatisha tamaa.

“Zamani wanawake wakisiasa walichukuliwa wahuni siyo kweli niwaambie huku katika  siasa kuna maendeleo mwanamke akisimama unajua ni kweli mwanaume anaweza leo kuegemea mashariki kesho yuko magharibi tuwaamini wanawake wamepewa uwezo mkubwa na wazazi tuunge mkono vipaji vya watoto wetu",alieleza Mwangwala. 

 

 

Post a Comment

0 Comments