ZIARA YA KWANZA YA MH;DEOGRATUS NDEJEMBI TANGU KUTEULIWA KUWA NAIBU WAZIRI YA KUTOA SHUKRANI KWA WAKAAZI WAKE::

 


Na Barnabas kisengi Chamwino 

Mbunge wa Jimbo la chamwino mkoani Dodoma ambaye pia ni Naibu Waziri Mteule wa Wizara ya Ofisi ya Rais Menejimenti utawala bora na utumishi wa umma Mh Deogratus Ndejembi amewaahidi wananchi wa Kata ya Segela kuwahakikishia atashirikiana nao katika kutatua changamoto zote zilizopo kwenye Kata hiyo kadri ya uwezo wake ili kuleta maendeleo katika Kata hiyo.

Ndejembi ameyasema hayo katika kijiji cha izava ambapo alikutana na wananchi wa Kata hiyo kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wa Jimbo la chamwino na kuwaeleza juu ya mikakati yake ya kuleta maendeleo Jimboni hapo na kwenye Kata zote 14 za jimbo la chamwino ambopo ndipo iliko ikulu ya Rais.

"niwashukuru wananchi wangu kwa kutupa kura nyingi Mimi binafsi na Rais na madiwani October mwaka huu sasa uchaguzi umekwisha na tayari tumesha apishwa na Mimi ndiye mbunge wenu sasa kwa kipindi cha miaka 5 najua tulikuwa na makundi mbalimbali katika kutafuta kura sasa naombeni Kama mlikuwa hamjavunja makundi sasa yavunjike na kuwe na kundi moja tu la chamwino yetu na maendeleo na sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa maendeleo binafsi na maendeleo ya chamwino tu"amesema Ndejembi 

"Ndejembi amesema kuwa wilaya ya chamwino ina majimbo mawili Jimbo la mvumi na Jimbo la chamwino sasa sisi tumebahatika Sana kuwa na ikulu ya rais pia hospitali kubwa ya uhuru na jirani hapa tunapakana na mji wa kiserikali ambapo wizara zote ziko hapo na ujenzi wa ofisi za mabalozi wa nchi zote unaendelea kujengwa hivyo wananchi wa Jimbo la chamwino twapasa kujivunia na kuhakikisha tunakuwa na maendeleo ya kasi na haraka" amesema Ndejembi.

Hii Ziara yangu nimeanzi hapa Segela ni kwa lengo la kuwashukuru pia nikuelekezana changamoto na mikakati ya ufumbuzi wa changamoto hizo na ninaendelea nayo kwa Kata zote 14 na mitaa yote vijiji na vitongoji kwa Jimbo zima niwahakikishie tu tupeane ushirikiano kuijenga chamwino mpya kwa maendeleo binafsi na maendeleo ya Jimbo na wilaya. 



Awali alipoingia katika Kata hiyo mbunge na naibu wazriri mteule alipokelewa na vikundi vya ngoma na bodaboda ndipo Ndejembi Naye akaonyesha umahiri wake wa kushuka kwenye gari na kupanda pikipiki na kuanza kuendesha hadi katika kijiji cha izava umbali wa kilometa 5 akiwa anaendesha pikipiki

Post a Comment

0 Comments