FOUNTAIN GATE YAWEKA WAZI MIPANGO YAKE,YATAMBULISHA WADHAMINI NA JEZI

 

 


📌RAMADHAN HASSAN

Timu ya Soka ya Wanawake ya Fountain Gate Princess imetambulisha jezi yake ya tatu huku  ikiweka wazi wadhamini  iliowapata kwa ajili ya kuidhamini timu katika Ligi kuu ya Soka ya wanawake.

Pia imesema mikakati yao ni kushika nafasi ya tatu katika Ligi kuu ya Soka ya wanawake inayoendelea   ambapo imedai  msimu ujao ni lazima  ichukue  ubingwa   wa Ligi hiyo.

Hayo yameelezwa leo Januari 18 2021 na Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Fountain Gate Academy,Japhet Makau  alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Makau amesema Fountain Gate imeamua kuingia kwenye michezo na eneo la kwanza ni katika mpira wa miguu ambapo amedai walianza na timu ya wanaume ambayo  kwa sasa inashiriki Ligi daraja la kwanza.

Amesema wameingia pia katika Soka la wanawake ambapo mwaka jana waliinunua timu ya Tanzanite na kwa sasa inaitwa Fountain Gate Princess ambayo inashiriki Ligi kuu ya Soka ya Wanawake.

Makau amesema Fountain Gate Princess ili  izidi kufanya vizuri ni lazima kuwe na  wadhamini wa kuweza kuiendesha timu hiyo iweze kujiendesha ambapo amewataja  wadhamini hao kuwa ni pamoja ni Kampuni ya Korie Super Rice ya Mkoani Morogoro,UBA Bank,Simba Nazi, na Jeff Solution ambao watasaidiana na Fountain Gate Academy.

“Ili tuweze kufanya vizuri lazima timu zetu ziwezeshwe na mfadhili mkuu wa timu yetu ni Fountain Gate Academy kwa timu zote,ili kuhakikisha tunaimarisha mchezo na vijana wanapata kile ambacho wanakihitaji tumeendelea kutafuta wadhamini wengine na wamekubali,tunao  Korie Super Rice ya Mkoani Morogoro na tutakuwa tunavaa jezi zenye nembo hiyo.

“Lakini pia tunao UBA Bank ambao wametoa ofa ya mchezaji bora wa mwezi pamoja na kila goli,wadhamini wengine ni Simba Nazi ya Jijini Dar es salaam na Jeff Solution,”amesema.

Mkurugenzi huyo amesema mikakati yao ni kushika nafasi ya tatu katika Ligi kuu ya Soka ya wanawake  msimu huu ambapo amedai  msimu ujao ni lazima  ichukue  ubingwa   wa Ligi hiyo.

Target yetu tunataka kuwa kwenye top three(nafasi ya tatu) mwaka ujao tutaingia kutaka kuwa mabingwa.

Makau


Katika hatua nyingine,Msemaji wa timu hiyo,Juma Ayo amewataja wachezaji saba wapya waliosajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya mikimiki ya Ligi Kuu  ya Soka ya wanawake huku akidai kwamba mchezo wa kesho wa ligi hiyo dhidi ya Baobao Queens wamejipanga kuondoka na pointi tatu.


Amewataja wachezaji hao na timu wanazotoka  katika mabano kuwa ni Aqwila Gasper  (Simba Queens) Stella Wilbart (Simba Queens) Saada Ramadhan (Simba Queens)Merry Masatu(Ruvuma Queens) Anna Ebron (Mlandizi Queens ) Zuhura Waziri (Ilala) na beki wa kulia Madelina Agostino (Ilala).

Amesema wachezaji hao watatumika katika mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Soka ya Wanawake dhidi ya Baobao Queens mtanange unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Fountain Gate Arena Jijini Dodoma.

Wachezaji wote hawa wanatumika katika kikosi chetu kwa sasa ni kizuri na kikosi kimekamilika.Kesho tuna mechi na Baobao Queens ni mechi muhimu sana.Nimeona mitandaoni watu  wanasema ni ‘Diarby’ sisi tuna kikosi kizuri waone kesho (Baobab Queens)  jinsi ya kupunguza mabao maana tutawafunga,mechi itaanza  saa 10 kesho hatutarajii kupata malalamiko yoyote,sisi kama Fountain Gate tupo vizuri tunaelekea kuwafunga.
 Ayo.

Post a Comment

0 Comments