KATIBU TAMISEMI DOKTA JOSEPH NYAMHANGA ATOA OMBI KWA SHULE BINAFSI.

 

📌RHODA SIMBA

KATIKA kipindi cha mwaka 2020/2021 serikali imetenga Sh. Bilioni 298 kwaajili ya mpango wa elimu bila malipo kwa shule za msingi.

 Hayo yamesemwa hii leo   jijini hapa na Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Pili wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania bara (TAPSHA).

Amesema katika  kuhakikisha elimu ya msingi hapa nchini inakuwa bora serikali itaendelea  kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni ili kukidhi haja ya wanafunzi na walimu

“Serikali iko makini kuhakikisha suala la elimu linakuwa mbele zaidi kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maboresho ya miundombinu katika ujenzi wa vyoo,vyumba vya madarasa, Nyumba  za walimu na mabweni,”alisema

Amesema mabadiliko makubwa yamefanyika  kwenye sekta ya elimu ya msingi ambayo yamechochewa na mpango huu wa elimu bure na ujenzi wa miundombinu hivyo ni wajibu wa walimu  kusimamia fedha hizo kufanya kazi iliyokusudiwa

 Katibu Mkuu huyo aliweka wazi kuwa Serikali inalaani vitendo vya udanganyifu wa mitihani na kuwataka walimu wakuu nchini kuendelea kudhibiti vitendo hivyo ili kuboresha elimu ya msingi.

“Ni jambo la kusikitisha kuona katika ulimwengu huu bado walimu hamuwezi kudhibidi wizi wa mitihani,tunawakatisha tama wanafunzi wanaojituma,.

Amesema “hata ninyi mtakuwa mashahidi kuwa tatizo la udanganyifu wa mitihani bado lipo na sereikali suala hili halitalifumbia macho  kwani kwa kipindi pekee cha mwaka jana jumla ya wanafunzi 1065 walifutiwa matokeo ya mitihani kwa udanganyifu,”alieleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa elimu Tanzania kutoka TAMISEMI ,Julius Nestory alitumia jukwaa hilo kuwataka walimu kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma  huku akisisitiza kuwa Serikali hatamvumilia mwalimu yeyote atakayekiuka agizo hilo.

Amesema siku za hivi karibuni yameibuka matukio ya baadhi ya wafanyakazi wa serikali wasio waadilifu kusambaza nyaraka za serikali kwenye mitandao ya kijamii na kusema jambo hilo ni kinyume na tarativu za utumishi wa umma.

Nestory amesema walimu wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii hivyo ni jukumu lao kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

“Matumizi ya mitandao ya kijamii hayaepukiki katika ulimwengu huu,lakini mnapswa kutumia kwa uangalifu bila kuharibu taaluma yenu,” alisema.

Awali,  Mwenyekiti wa Umoja wa walimu hao(TAPSHA)Rehema Ramole  alisema  mkutano huo utasaidia mafunzo mbalimbali ya uongozi, haki na wajibu wao na kukabiliana na rushwa.

Mwenyekiti huyo  (TAPSHA) ambaye pia ni Mwalimu wa Shule ya msingi Makuburi Jeshini Ubungo jijini Dar es Salaam alieleza kuwa wao kama wakuu wa shule wanao wajibu wa kukumbushana na kukemea vitendo vya rushwa na kuendelea kuiunga mkono serikali dhidi ya kukomesha vitendo vya rushwa na uvujaji mitihani  mashuleni.

“Tupo pamoja na Serikali yetu katika kukuza elimu nchini,Kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni uongozi na usimamizi makini wa elimu utaimarisha na kuiendeleza Tanzania katika uchumi wa kati inaonyesha wazi ni kwa jinsi gani tupo tayari kupokea maagizo yoyote yanayotolewa na serikali yenye lengo la kuinua elimu,”amesema.

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments