MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAONGEZEKA HADI ASILIMIA 3.2% KUTOKA ASILIMIA 3.0%.


📌
DEVOTHA SONGORWA.

Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia Mwezi Disemba ,mwaka Jana  umeongezeka hadi asilimia 3.2% kutoka asilimia 3.0% kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba mwaka Jana.

Hayo yamebainishwa Leo Januari 8,2021 jijini Dodoma Mkurugenzi wa Sensa ya watu na takwimu za jamii Bi.Ruth Minja wakati akizungumza na waandishi wa Habari.

Amesema hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2020 imeongezeka kidogo  zikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2020.

 Aidha,Bi.Minja amebainisha kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba ,2020 kumechangiwa kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Disemba 2020 ikilinganishwa na bei za Mwezi Disemba 2019.

Bi.Minja ameainisha baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi Disemba 2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Disemba 2019 ni pamoja na nyama kwa asilimia 3.1%,samaki wabichi asilimia 15.6%,mayai kwa asilimia 3.0%,dagaa kwa asilimia 13.2%,mafuta ya kupikia kwa asilimia 9.0%,matunda kwa asilimia 16.9%,maharage kwa asilimia  6.2%,choroko kwa asilimia 12.0%,viazi mviringo kwa asilimia 5.5%,na mihogo kwa asilimia 13.5%.

Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi Disemba 2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Disemba 2019 ni pamoja na nguo za wanaume  kwa asilimia  3.9%,nguo za wanawake kwa asilimia 2.0%,gesi ya kupikia kwa asilimia 7.1%,na Mkaa kwa asilimia 12.3%.

Pia ,Bi Minja amesema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji Baridi kwa mwezi Disemba 2020 umeongezeka hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2020  .

Kuhusu wastani wa mfumuko wa bei wa taifa  kutoka mwezivJanuari  hadi Disemba  2020 Bi.Minja amebainisha kuwa umepungua hadi asilimia 3.3% mwaka 2020 kutoka asilimia 3.4% mwaka 2019(kutoka mwezi Januari hadi mwezi Disemba 2019).

Hivyo,Wastani wa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula umeongezeka hadi asilimia 5.0% kwa mwaka 2020 kutoka asilimia 4.3%  kwa mwaka 2019.

Na wastani wa bei jumuisha bidhaa za vyakula na Nishati umepungua hadi asilimia 2.3% mwaka 2020 kutoka asilimia 3.0% mwaka 2019.

Post a Comment

0 Comments